Balozi wa Norway Nchini Tanzania Mhe.Tone Tinnes amezindua Jengo la kikundi cha Wosia wa Baba Machi 14,2024 ambalo limejengwa kwa ufadhili wa EAMCEF kwa Hisani ya Serikali ya Ufalme wa Norway.
Kikundi kilianza Mwaka 2006, kina Jumla ya Wanachama 20 ambapo kinapatikana Kijiji cha Msufini, Kata ya Mkula katika Halmashauri ya Mji Ifakara.
Kikundi hicho Hujishughulisha na uchakataji na uuzaji wa Mazao ya Nyuki kama Asali,Nta na mengineyo.
Hadi kufikia Mwaka 2023 kikundi kimeweza kuzalisha zaidi ya Lita 400 za Asali na kuweza kujipatia kipato kwa Mtu mmoja mmoja na kupunguza tatizo la ukosefu wa Ajira.
Ikumbukwe kwamba Norway na Tanzania ni Nchi zilishobina kwa Miaka 60 sasa na Kushirikiana katika sekta tofauti tofauti za kiuchumi na Jamii.
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: -
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa