Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara Bi.Zahara Michuzi amefanya kikao na Wakala wa Majengo - TBA leo Januari 31,2024.
Lengo la Kikao hicho ni kufanya makubaliano ya namna gani ujenzi wa Jengo la Utawala litaendelea kujengwa na kufikia hatua nzuri ambapo Watumishi wataweza kukaa na kuepukana na adha ya kujibana katika Ofisi ya zamani yenye uchache na ufinyu wa vyumba vya Ofisi.
Hata hivyo Meneja wa TBA Mkoa wa Morogoro Eng.Rebeka Kimambo, amemuhakikishia Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kuwa ujenzi utaanza mapema mwezi ujao mara baada ya ununuzi wa vifaa vya Ujenzi kukamilika.
Ikumbukwe kuwa Jengo Hilo lilianza kujengwa Mwaka 2018 na Ujenzi ulisimama kwa zaidi ya Mwaka mmoja Hadi sasa.
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: -
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa