Madiwani na Wataalam wa Halmashauri ya Mji Ifakara, wamefanya Ziara ya kutembelea baadhi ya Halmashauri zilizopo ukanda wa Nyanda za juu Kusini mwa Tanzania.
Lengo la Ziara hiyo ni kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo; Utawala,Kilimo cha Kokoa na Parachichi, mbinu mbalimbali za kuanzisha na kuendesha Vyanzo vya Mapato sambamba na mbinu za Ukusanyaji Mapato bila kusahau usafi wa Mazingira.
Ziara hiyo iliyoongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Ifakara Mhe.Kassim Nakapala ilianza Aprili 15,3024 katika Halmashauri ya Wilaya ya Kyela Kisha Halmashauri ya Mji Njombe na kumaliziwa katika Halmashauri ya Mji Makambako.
Katika Halmashauri ya Wilaya ya Kyela wameweza kujifunza Kilimo cha Kakao,kuanzia upandaji, utunzaji,uvunaji,uhifadhi na uuzaji.
Hata hivyo katika Halmashauri ya Mji Njombe wamepata ujuzi wa uendeshaji wa Mradi wa Soko na Kilimo cha Parachichi sambamba na utunzaji wa usafi wa Mazingira.
Kwa kumalizia Aprili 17,2024 katika Halmashauri ya Mji Makambako Wameweza kujifunza uendeshaji wa Mradi wa Ufyatuaji Tofali ambapo hivi karibuni Halmashauri ya Mji Ifakara imeanzisha Mradi huo.
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: -
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa