IFAKARA MJI YATWAA KOMBE LA MSHINDI WA PILI, SHIMISEMITA 2024
Timu ya Mpira w Miguu wanaume ya Halmashauri ya Mji Ifakara imetwaa kombe la Mshindi wa Pili kwenye hatua ya fainali ya SHIMISEMITA 2024 baada ya kufungwa kwa taaabu sana na Timu ya Geita DC goli 2 kwa moja hapo jana Alhamisi tarehe 5 Septemba, 2024.
Akizungumza mara baada ya ushindi huo Afisa Michezo wa Halmashauri ya Mji Ifakara Bwana Rashid Mgaruka alimshukuru Mungu kwa ushindi huo kwani kazi haikuwa rahisi. Vile vile amemshukuru Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara Bi. Zahra Michuzi kwa kuwawezesha kushiriki mashindano hayo yaliyowafanya kukutana na marafiki na pia kutengeneza marafiki wapya. Bwana Mgaruka aliahidi timu kuendelea kujipanga vizuri kwaajili ya mashindano yajayo.
" Tunamshukuru Mkurugenzi wetu wa Halmashauri ya Mji Ifakara Bi. Zahra Michuzi ambaye ni mwanamichezo namba moja kwa kutuwezesha kushiriki mashindano haya kwani tumeweza kufahamiana na watu na kuongeza jiografia ".alisema Bwana Mgaruka na kuongeza " tumepata fursa ya kurefresh na hivyo tunarudi kazini tukiwa na nguvu na ari mpya. Tunaahidi safari nyingine kubeba kombe la Mshindi wa kwanza." alimaliza Bwana Mgaruka
Jumla ya timu 66 zilishiriki mashindano hayo ya SHIMISEMITA 2024 yaliyofanyika Jijini Mwanza kuanzia tarehe 25 Agosti, 2024 na kuhitimiswa jana Septemba 5, 2024.
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: -
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa