Wafugaji wa Kijiji cha Nyange kilichopo Kata ya Msolwa Station katika Halmashauri ya Mji Ifakara wamehamasishwa kushiriki na kutambua umuhimu wa siku ya Wanawake Duniani itakayoadhimishwa tarehe 8 Machi Duniani kote na kujitokeza kushiriki zoezi la kuboresha taarifa zao katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura linalotarajiwa kuanza tarehe 1 hadi 7 Machi Jimbo la Kilombero .
Hamasa hiyo imetolewa leo tarehe 27 Februari 2025 na Diwani wa Viti Maalum Tarafa ya Mang'ula Mhe. Petronila Mayombo , Diwani wa Viti Maalum Tarafa ya Kidatu Mhe. Emma Ngunga pamoja na Afisa Maendeleo ya Jamii ambaye ni Mratibu wa Dawati la Jinsia wa Halmashauri ya Mji Ifakara Bw. Agano Mtweve ambapo waliwaelemisha juu ya Matukio hayo ambapo kwa Mkoa wa Morogoro sherehe hiyo itaadhimishwa katika Halmashauri ya Mji Ifakara Viwanja vya CCM Tangani au Uwanja wa Taifa - Ifakara ambapo Mgeni Rasmi atakua Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima.
Aidha kwa upande wa Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Jamii hiyo ilielezwa kuwa Vituo vitakua wazi kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 12:00 Jioni katika Kata zote 19 kwenye Vijiji , Mitaa na Vitongoji .
Mmoja wa Wafugaji hao Bibi. Rehema Samato aliwashukuru Viongozi hao kwa kuwafikia katika Maeneo yao Ili waweze kushiriki katika matukio hayo muhimu kwa Taifa na kuahidi kuwa jamii hiyo itashiriki vizuri.
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: -
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa