HALMASHAURI YA MJI IFAKARA YANUNUA GARI KWAAJILI YA KUZOA TAKA NA KUWEKA MJI SAFI
Halmashauri ya Mji Ifakara imenunua Gari kwaajili ya kubeba taka na kuweka Mji Safi. Gari hilo limezinduliwa Jumatatu tarehe 22 Septemba 2025 na Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Mhe. Wakili Dunstan Kyobya nje ya Ofisi za Halmashauri ya Mji Ifakara.
Awali Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara Bi. Pilly Kitwana alieleza kuwa Gari hilo limenunuliwa kutokana na Mapato ya ndani ya Halmashauri na Bajeti hiyo ilipangwa ili kuondokana na adha iliyokuwepo awali ya uzoaji taka.
Wakati huohuo Mkuu wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Bw. Rashidi Semngoya alisema kuwa kutokana na ujio wa gari hilo lenye uwezo wa kubeba taka nyingi kwa wakati mmoja alitoa wito kwa wananchi wa Ifakara kuhifadhi taka kwenye vyombo mahususi ili taka hizo ziweze kuchukuliwa kirahisis na watoe ada /tozo za taka bila shuruti.
" Ninaamini Gari hili tutalitumia na kulitunza vizuri ili liweze kutoa huduma kwa kipindi kirefu zaidi na kuhakikisha Mji wetu unakua safi muda wote ". Alisisitiza Bwana Semngoya.
Nae Mkuu wa Kitengo cha Usafi na Udhibiti wa Taka ngumu Bw. Gabriel Malisa alieleza jinsi Mji utakavyokuwa Msafi kwani hii ni nyenzo muhimu na wananchi wanapaswa kuchangia kulipa ada za taka ili huduma hiyo iendelee kuwa nzuri.
Kwa upande wake Mgeni Rasmi wakati wa Hafla hiyo ya Uzinduzi Mhe. Wakili Dunstan Kyobya alisisitiza kuendelea kutolewa kwa Elimu ya Usafi wa Mazingira kwa Wananchi wa Halmashauri ya Mji Ifakara katika ngazi za Mtaa, Vijiji, Vitongoji, na Taasisi zote.
" Changamoto ya Usafi wa Mji ilikuwa kubwa sana , uwepo wa Gari hiii utakuwa Muarobaini wa kwenda kuondoa uchafu wote katika maeneo yote na kila Duka liwe na chomboo cha kuhifadhia taka ". Alisema Mhe. Kyobya.
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: -
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa