Wananchi wa Halmashauri ya Mji Ifakara leo Disemba 1, 2024 wameshiriki katika kuadhimisha siku ya Ukimwi Duniani inayoadhimishwa Duniani Kote kila ifikapo Disemba, 1 ya kila mwaka.
Maadhimisho hayo yamefanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Lumemo vilivyopo Halmashauri ya Mji Ifakara ambapo Mgeni Rasmi alikua Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Mhe. Wakili Dunstan Kyobya ambapo aliitaka jamii kutokuwatenga watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi badala yake kushiriki kuwalinda kuwatunza na kuwasimamia ikiwemo kuwawezesha katika kujikwamua kiuchumi.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara Bibi. Witness Kimoleta aliitaka jamii kuzidi kujikinga dhidi ya Maambukizi mapya na wale waliogundulika na virusi hivyo kuzingatia matumizi Sahihi ya dawa.
Aidha Takwimu zinaonesha mpaka sasa watu zaidi ya elfu 10,000 wanaishi na Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi Halmashauri ya Mji Ifakara.
Aidha kauli mbiu katika maadhimisho hayo ilikua ni " Chagua njia Sahihi tokomeza Ukimwi".
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: -
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa