Halmashauri ya Mji Ifakara Imeadhimisha miaka 63 ya Uhuru kwa Kupanda miti elfu 10 katika Kata ya Mbassa.
Tukio hilo limeongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Mhe.Wakili Dunstan Kyobya ambapo miti hiyo ilipandwa kando ya mto Lumemo uliopo Kata ya Mbasa.
Aidha Mkuu huyo wa Wilaya alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha Kwa ajili ya ujenzi wa tuta la kuzuia maji ya Mto Lumemo kwenda kwenye makazi ya watu na kusababisha mafuriko.
" Leo tumepanda miti kando ya Mto Lumemo ikiwa ni maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Kwamba kila Wilaya,Kila mwananchi Kupanda mti siku ya 9 Disemba kama uhifadhi wa mazingira hivyo niziombe taasisi zingine kuja kupata maeneo ya kutengeneza garden kuanzia daraja la Machipi mpaka Lipangalala kuwe na maeneo ya kuvutia."Amesema Mhe.Kyobya
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara Bibi. Witness Kimoleta aliutaka uongozi wa Kata ya Mbassa kuitunza miti hiyo ili kuhakikisha inakua vizuri.
" Afisa Maendeleo ya Jamii ahakikishe miti inapandwa katika Eneo hili na pia nitoe wito na niagize Serikali ya Kijiji na Kata ya Mbassa kuhakikisha Ulinzi na usalama wa maeneo haya yaliyokwisha pandwa miti ili iweze kukua vizuri". Alieleza Bibi. Kimoleta.
Nae Katibu Tawala wa Wilaya ya Kilombero Bw. Abraham Mwaikwila aliwasihi Wananchi kushiriki shughuli za Kijamii katika maeneo mbalimbali ikiwemo Kupanda miti, kufanya usafi sehemu mbalimbali.
" Ifakara tuna NGOs nyingi ambazo zina jihusisha na Uhifadhi wa Mazingira hivyo niwasihi wazidi kujitokeza kupata maeneo ya kupanda miti ili kutunza Mazingira yetu. Alisema Bw. Mwaikwila
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: -
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa