Mradi huo ulitekelezwa katika Shule nne za Halmashauri ya Mji Ifakara ambazo ni Miembeni, Katindiuka , Kining'ina na Kibaoni ambapo ulianza kutekelezwa mwaka 2018 hadi 2022 na Taasisi ya Afya Ifakara -( IHI) kwa kushirikiana na Wafadhili kutoka Uswizi ( Swiss Tropical and Public Health Institute).
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa taarifa hiyo Jumatano tarehe 29 /1/2025 , Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara Dkt. Yuda Mgeni aliipongeza Taasisi hiyo kwa taarifa hiyo kwani itasaidia jamii katika kuhakikisha watoto wanakua katika Mazingira mazuri ya kusoma na afya bora .
" Niwapongeze kwa kazi nzuri ya utafiti ambapo matokeo utafiti huu yatasaidia Halmashauri katika kuboresha elimu na ufaulu mashuleni kwa kuhimiza mazoezi kwa wanafunzi na kuhimiza wazazi kuhusu umuhimu wa chakula kwa wanafunzi mashuleni ". Alisema Dkt. Yuda
Aidha , Mradi huo ulitekelezwa katika nchi tatu za Afrika Kusini, Ivory Cost na Tanzania - Wilaya ya Kilombero lengo ikiwa ni kuchunguza umuhimu wa Mazoezi ya Viungo na Virutubisho vya ziada katika ukuaji na Maendeleo ya watoto walioko mashuleni .
Mmoja wa Wanasayansi Watafiti wa Taasisi ya Afya Ifakara (IHI) Bi. Eliahika Minja alisema katika Utafiti huo walibaini mambo mbalimbali ikiwemo watoto wengi kutokupata mlo kamili kwa kuzingatia makundi ya chakula au kupata mlo mmoja hali inayochangia udumavu na kuwa na uwezo mdogo wa kufikiri au kushindwa kushiriki Michezo au mazoezi ya viungo, hivyo alisisitiza Elimu izidi kutolewa kwa jamii kuzingatia kuwapa watoto chakula hasa kwa makundi yote ya chakula ili kuongeza uwezo wa kusoma wawapo mashuleni na kusisitiza vipindi vya michezo vihusishe wanafunzi kufanya mazoezi na kucheza Michezo mbalimbali.
Mradi huu ulihusisha jumla ya wanafunzi 1,055 kutoka shule hizo ambapo wasichana 543 na wavulana 494 .
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: -
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa