Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe.Doto Biteko amezindua Kituo cha kupoza umeme Mei 31,2024 kilichopo Kata ya Kibaoni katika Halmashauri ya Mji Ifakara.
Kituo hicho kilichoanza kujengwa Machi 2020 kimegharimu kiasi cha Shillingi Bilioni 24.5 ambapo ufadhili wa Jumuiya ya Ulaya kupitia Mfuko wa Maendeleo wa Umoja wa Jumuiya ya Ulaya (European Development Fund - EDF) kwa ajili ya kuunga Mkono jitihada za Serikali za kuondoa umaskini katika kuendeleza Kilimo katika ukanda maalum ujulikanao kama SAGCOT kwa kuchangia Shilingi Bilioni 18 na Serikali ya Tanzania kuchangia Shilingi Bilioni 6.59.
Hata hivyo Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe.Adam Kighoma Malima amesema kwakuwa kituo hicho ni mahususi kwa Wakazi wa Kilombero ,Malinyi na Ulanga anaimani na ongezeko na Pato la Mkoa huo kwan kuondoka kwa tatizo la kukatika umeme ni chachu ya uzalishaji katika Shughuli za kiuchumi.
Miongoni mwa manufaa ya kituo cha kupoza umeme ni pamoja na kuondoa adha ya kukatika katika kwa umeme majumbani, ongezeko la Ajira na urahisishaj wa uzalishaji wa bidhaa mbalimbali zinazotumia umeme kama ukoboaji wa Mpunga.
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: -
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa