Baadhi ya Askari wa jeshi la Polisi Tarafa ya Mang'ula Kata ya Mwaya katika Halmashauri ya Mji Ifakara wanaishi katika nyumba chakavu hali ambayo inahatarisha maisha yao.
Akizungumzia suala hilo Diwani wa Kata ya Mwaya Mhe.Antony Mwampunga amesema kuwa mazingira wanayoishi polisi hao sio rafiki kwani nyumba hizo zinaweza kuanguka wakati wowote
"Pale wanapo ishi sio Salama na sisi tupo tayari kufyatua tofali ili tuwajengee polisi nyumba." amesema Mhe.Mwampunga na kuongeza kuwa Eneo ambalo kwa sasa wanaishi polisi wa kata hiyo lipo chini ya TAZARA hivyo watafutiwe eneo la kudumu ili waweze kujenga nyumba zenye ubora.
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: -
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa