Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Mhe. Wakili Dunstan Kyobya leo Jumatatu tarehe 28 Oktoba 2024 amezindua Wodi ya kujifungulia wakina mama wajawazito katika Kituo cha Afya Kibaoni kilichopo Halmashauri ya Mji Ifakara pamoja na Vifaa tiba ikiwemo Kiti cha Kung'olea meno ( Dental Chair) , mashine ya kufulia pamoja na Mashine ya Mionzi (X Ray).
Aidha alimshukuru Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuleta kiti cha kisasa cha kung' olea meno chenye thamani ya Shilingi Milioni 21, Mashine ya kufulia yenye thamani ya Shilingi Milioni 22, pamoja na Mashine ya mionzi (X Ray) yenye thamani ya Shilingi Milioni 566.
Vile vile, Mhe. DC alimshukuru Mdau SOLIDARMED kwa kukarabati wodi ya Kujifungulia kina mama na pia alimshukuru Mbunge wa Jimbo la Kilombero Mhe. Abubakari Asenga kwa kusaidia upatikanaji wa Vitanda katika wodi hiyo ya kina mama.
" Shukrani kwa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt . Samia Suluhu Hassan kwa kutuletea vifaa tiba hivi, kwani vitatatua changamoto nyingi katika Hospitali hii hivyo kila mtumiaji , wagonjwa na wanaifakara kwa ujumla tunapaswa kuvitunza ili viendelee kutusaidia ". Alisema Mhe. Kyobya
Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Kituo hicho Daktari Dorcas Ng'wandu alishukuru kwa upatikanaji wa Vifaa hivyo na kuahidi kuvitumia vizuri.
Aidha Mhe. Kyobya alitumia nafasi hiyo kumpongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara Bi .Zahara Michuzi kwa kusimamia vizuri Utekelezwaji wa miradi mbalimbali ya Maendeleo katika Halmashauri hiyo.
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: -
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa