Mkuu wa Wilaya ya kilombero Mhe.Wakili Dunstan Kyobya amefika kata ya Lipangalala Oktoba 31/2024, nyumbani Kwa Bi. Selestina Akwera ambaye alikuwa na mgogoro wa ardhi na Bw. Sikujua Funuki uliodumu kwa zaidi ya miaka 5.
Dc Kyobya alisisitiza suala la amani kufuatia amri iliyotolewa na mahakama ya kugawana Kwa sehemu ya ardhi hiyo Kwa pande zote mbili na kuwataka kumaliza tofauti zao Kwa kuweka mipaka na Kila mmoja abaki na eneo lake bila kubughudhiwa.
Aidha Dc Kyobya ametoa siku saba Kwa Watendaji wa kata ya Lipangalala na Lumemo kuweka utaratibu mzuri wa kwenda kuhakikisha agizo hilo linafanyiwa kazi kama amri ya Mahakama inavyosema.
"Nataka amani iwepo, bado Bibi Salome una ekari 24 na funuki una ekari 12, Kila mmoja aheshimu makubaliano naelekeza uongozi wa Tarafa, Kata ya Lipangalala na Lumemo mfike eneo husika mkaweke mipaka Kwa mujibu wa makubaliano,"Amesema Dc Kyobya.
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: -
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa