Kampeni hiyo imezinduliwa leo tarehe 19 Novemba na Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Mhe. Wakili Dunstan Kyobya katika Shule ya Sekondari Katurukila iliyopo Kata ya Mkula Halmashauri ya Mji Ifakara.
Akizungumza mara baada ya kupanda mti katika shule hiyo Mkuu wa Wilaya alisisitiza wanafunzi , walimu pamoja na Wananchi wote wa eneo hilo kuitunza miti hiyo ambayo itasaidia kukabiliana na Mabadiliko ya tabia ya nchi.
" Miti hii itunzwe jumla ya Miti 600 inatarajiwa kupandwa hapa , tutapata matunda , kivuli na kutunza mazingira yetu kwa ujumla". Alieleza Mhe. Kyobya
Aidha tukio hilo lilitanguliwa na matembezi kutoka Ofisi ya Kijiji mpka shule ya Sekondari Katurukila.
Kwa upande wake Mkuu wa Shule hiyo Bw. Kassim Mandwanga alimshukuru Mkuu wa Wilaya kwa kushiriki zoezi hilo la Upandaji wa Miti ambapo aliahidi shule hiyo kwa kushirikiana na Wananchi wa Kijiji hicho kuendelea kuitunza miti hiyo na kuahidi shule hiyo kufanya vizuri.
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: -
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa