Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Mhe.Wakili Dunstan Kyobya ametoa Masaa 72 kwa wataalamu wa Ardhi kupima na kuhakiki nyaraka zote za umiliki wa Ardhi baina ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI )- KATRIN na Wananchi wa Kitongoji cha Igombati kilichopo Kijiji cha Lumemo Halmashauri ya Mji Ifakara.
Hayo ameyasema leo tarehe 13 Novemba 2024 alipokuwa akisikiliza na kutatua Mgogoro wa Ardhi baina ya Wananchi wa Kitongoji cha Igombati na TARI - KATRIN.
Awali, mmoja wa Wanakijiji Bw. Lucian Mwangaitema alisema tangu azaliwe miaka 73 iliyopita wamekuwa wakitumia eneo hilo kwa Kilimo na hajawahi kuona Shirika au Kampuni yoyote inadai eneo hilo.
Kwa upande wake Bw. Abdallah Mpunga kutoka TARI - KATRIN alisema eneo hilo linamilikiwa na Taasisi hiyo tangu wakati TARI inaitwa Tanganyika Agricultural Corporation (TAC ) iliyoanzishwa mwaka 1954.
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: -
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa