BODI YA PAMBA TANZANIA YAFANYA UWEKEZAJI ENEO LA KIJIJI CHA KIKWAWILA LENYE UKUBWA WA EKARI ELFU 11,000 KWAAJILI YA KILIMO CHA DENGU
Bodi ya Pamba Tanzania imefanya Uwekezaji wa Kilimo cha zao la Dengu katika Eneo la Shamba la Kijiji cha Kikwawila , Muomakila lililopo Kata ya Kibaoni kwa kipindi cha Miezi Minne kuanzia Mwezi Agosti hadi Novemba 2025 ambapo Shamba hilo huwa halitumiwi na Wanakijiji kwa muda huo huwa wameshavuna Mazao yao ambayo ni Mpunga na kusubiri msimu mwingine wa Kilimo ambacho huanza Mwezi Novemba . Aidha Mwekezaji huyo atatumia Shamba hilo kwa Kipindi ambacho Shamba linakuwa halina shughuli zozote za kilimo kwa Wanakijiji kwa muda wa miezi 4 kwa Gharama ya Shilingi Milioni 50,000,000 ambapo Fedha hiyo itawekwa katika akaunti ya Kijiji.
Akizungumza wakati wa Mkutano wa Wanakijiji cha Kikwawila , Viongozi wa Serikali ya Kijiji, Halmashauri , Wilaya na Wawekezaji hao tarehe 20/7/2025, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima aliwaeleza Wanakijiji hao kuwa mbali na Mwekezaji huyo kukodi Ekari hizo pia atawalimia Wananchi Ekari Elfu 2,000 kati ya Ekari Elfu 11,000 anazozikodi na kwamba Wananchi hao Watazisimamia na kuwa mfano kwa wengine.
"Ekari Elfu 11 zitalimwa kati ya hizo Ekari Elfu 2 zitalimwa kwaajili ya Wanakijiji kila mtu atapewa azisimamie kwenye utaratibu wa Ushirika wa Kijiji, Ekari elfu 9 zitakuwa kwaajili ya Mwekezaji ". Alisema Mhe. Malima
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Pamba Aggrey Mwanri alisema katika Uwekezaji huo Wanakijiji hao watanufaika ambapo Bodi ya Pamba itachangia shughuli za kimaendeleo kwa Kijamii kama ELIMU , Afya , Miundo Mbinu n.k
Mmoja wa Wananchi wa Kijiji hicho Bw. Martine Ngwega alieleza ujio wa Mwekezaji katika Eneo hilo utanufaisha Wananchi wa Kijiji hicho kwani Kipindi ambacho wanakuwa wamevuna Mpunga eneo hilo linakuwa halitumiki hivyo kuja kwa Mwekezaji huyo kutaendelea kuongeza mapato na Ustawi wa Kijiji hicho.
"Tunashukuru Mwekezaji kwa kulichagua eneo letu, kwani pia suala la Miundombinu ameahidi kututengenezea na Vijana wetu watapata Ajira kupitia Uwekezaji huu". Alisema Bw. Ngwega
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: -
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa