Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati,Mhe.Dkt Doto Biteko, amefanya Ziara katika Kituo cha kuzalisha umeme Kidatu Ifakara Wilayani Kilombero leo Aprili 1,2024.
Ziara hiyo ni kutokana na kukatika kwa Umeme Nchi nzima kutokana na kuzima kwa Gridi ya Taifa hali ambayo imesababishwa na hitilafu katika Mitambo ya umeme ikiwa chanzo chake ni Mvua Kubwa zinazoendelea.
Hata hivyo Dkt.Biteko amewataka Wananchi kutokuwa na wasiwasi wa kuendelea kwa hali hiyo kwani Matengenezo ya urekebishaji wa Mitambo yanaendelea."Hali hii ni hitilafu katika Mitambo ya umeme na TANESCO wanashughulikia kwa uharaka na umakini ili kuwaondolea adha Watanzania, niwahakikishie Watanzania wenzangu kuwa kwa sasa hakuna Mgao wa umeme" Amesema Dkt.Biteko.
Sambamba na hayo Biteko amewataka Wataalam wa TANESCO kufanya marekebisho haraka iwezekenavyo kufanya marekebisho haraka iwezekenavyo mara tu hitilafu ya umeme inapojitokeza ili kuepusha hasara kwa Watanzania hasa ambao shughuli zao za Kiuchumi zinategea Nishati hiyo.
Akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe.Kighoma Malima, Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Mhe.Dunstan Kyobya Ameahidi kusimamia Miundombinu ya kituo hicho ili kuepusha adha ya aina yoyote inayohusu umeme kwa Wananchi.
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: -
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa