Imeelezwa kuwa ufaulu wa Mtihani wa darasa la saba kwa mwaka 2017 katika shule za Msingi za Halmashauri ya Mji Ifakara umeongezeka kutoka 65.3% ya mwaka 2016 hadi 73.35% mwaka 2017 sawa na ongezeko la 8.05% na kupelekea kupanda hadhi ya elimu ya Msingi ya Halmashauri kitaifa kwa kushika nafasi ya 84 kutoka nafasi ya 121 ya mwaka jana
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Idara ya elimu Msingi wa Halmashauri ya Mji Ifakara Bi.Mariam Nnauye wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu maandalizi ya Mtihani wa Upimaji wa kitaifa wa darasa la nne utakaoanza kesho Novemba 22 na kumalizika Novemba 23, 2017 kwa shule zote Tanzania
Bi Nnauye amefafanua kuwa pamoja na kuwa Halmashauri kushuka kwa nafasi moja Kimkoa ambapo mwaka huu imekuwa katika nafasi ya 5 lakini idadi ya Wanafunzi waliofaulu ni kubwa tofauti na mwaka 2016. Jumla ya Wanafunzi 2415 walifanya mtihani mwaka jana lakini waliofaulu walikuwa 1577 wakati mwaka huu waliofanya mtihani walikuwa 2642 na jumla ya Wanafunzi 1938 walifaulu na hivyo idadi hiyo kuzidisha ufaulu kwa 8.05% tofauti na mwaka jana na kupelekea kupandisha nafasi ya ufaulu Kitaifa
Akizungumzia Mitihani ya upimaji wa kitaifa kwa darasa la nne, Afisa Elimu Msingi amesema kuwa wana matarajio mazuri pia kwani maandalizi yako vizuri na Wanafunzi wameandaliwa kufanya mitihani hiyo kikamilifu. Jumla ya Wanafunzi 3116 wamesajiliwa kufanya Mtihani huo kwa mwaka huu kwa shule zote za Serikali na binafsi ambapo Wavulana ni 1542 na Wasichana 1574.
Watahiniwa wote waliosajiliwa kufanya Mitihani ya upimaji wa kitaifa kwa darasa la nne wataanza mitihani yao kesho kwa shule 39 za Halmashauri ya Mji ambapo kati ya hizo 33 ni za Serikali na 06 ni shule binafsi. Hata hivyo Kituo cha Ufundi kilichopo shule ya Msingi Mlabani wameanza mitihani yao leo.
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: -
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa