Mawakala wa vyama mbalimbali vilivyosajiliwa katika Halmashauri ya Mji Ifakara wakipata semina fupi kuhusu zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la kudumu la wapiga kura ,pamoja na kujua majukumu yao pindi watakapokuwa katika vituo vya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura.
Pia zoezi hili litadumu kwa muda wa siku saba ,kuanzia tarehe 03/02/2020 hadi 09/02/2020 .Vituo vyote vitafunguliwa kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni.
Wakazi wote wa Ifakara kwa wale watakaofikisha umri wa miaka kumi na nane(18) kabla ya siku ya kupiga kura ,na kwa wale ambao wanataka kubadilisha vituo vya kupigia kura na ambao wamepoteza kadi zao , wote mnatakiwa kufika vituoni .
Kumbuka ukikosa kitambulisho cha kupigia kura utakuwa umekosa haki yako ya msingi ya kupiga kura ya kuchagua Diwani ,Mbunge na Raisi katika uchaguzi wa Oktoba 2020.
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: -
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa