Wafanyakazi wa TANSCO wamepigwa marufuku kukaa ofisini na kusubiri wateja wawafate na kutakwa wao kuwafuata wateja ili waweze kuwapatia huduma bora.
Marufuku hiyo imepigwa na Waziri wa Nishati na Madini Mh. Athanasi Nangari alipokuwa anazindua jengo la TANESCO la Wilaya ya Kilombero lililopo katika Halmashauri ya Mji Ifakara, Jengo ambalo limegharimu kiasi cha Tsh. 270,298,167.25. ambazo ni fedha za ndani.
Kwa upande mwingine Mh. Nangari ameahidi kuanza kwa ujenzi wa Substation yaani kituo cha kupooza umeme ndani ya Halmashauri ya Mji wa Ifakara mwezi ujao ambayo itasaidia kuimalisha upatikanaji wa umeme na kupunguza kukatika kwa umeme mara kwa mara.
Pamoja na hilo Mh. Waziri ameitaka TANESCO kuongeza mapato yake na kuhakikisha inawafatilia wadaiwa sugu wote Ili waweze kulipa madeni yao.
Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Ndg. James Ihunyo ameipongeza TANESCO kwa ujenzi huo kwani utasaidia kuwahudumia wananchi, Pia amemuomba Mh. Waziri asaidie kujenga kituo cha kupooza umeme kwa muda mfupi ili kuweza kusaidia kupatikana kwa umeme wa uhakika kwani Halmashauri ya Mji Ifakara inaongezeo mkubwa sana la idadi ya Viwanda hivyo umeme wa uhakika unahitajika.
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: 0738 223 543
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa