Mfuko wa hifadhi ya jamii NSSF umefanya semina na viongozi wa vikundi vya wajasiriamali Halmashauri ya mji ifakara ilikutoa elimu juu ya sheria namba 2 ya mwaka 2018 inayo upa mamlaka mfuko huo ya kuhudumia watu wa sekta zisizo rasmi iliwanufaike na mafao yanayo tolewa na mfuko huo.
Hayo yameelezwa leo na Afisa muandamizi wa NSSF Ndugu Salaha Magumbala wakati wa semina hiyo iliyofanyika ukumbi wa mazingira uliopo kata ya kibaoni katika Halmashauri ya mji Ifakara .Ambapo ame fafanua kuwa sheria hiyo imepitishwa na bunge tarehe 08/02/2018 na kusainiwa na Raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli tarehe 09/02/2018 na kuanza kutumika rasmi tarehe 1/08/2018 baada ya kutangazwa na waziri mwenye dhamana Mh Jenista Muhagama ili kuhakikisha wananchi wanapata hifadhi ya jamii.
Aidha amesema kuwa mafao yanayo tolewa na mfuko wa NSSF ni ya aina mbili mafao ya muda mrefu na muda mfupi .mafao ya muda mrefu ni mafao ya uzee, ulemavu,na urithi mafao ya muda mfupi ni uzazi, matibabu,msaada wa mazishi ambapo sheria hii imeunganisha mifuko 4 PAPF,PSPF,GPF,LPF na kuwa mfuko mmoja yani PSSP ambao ni mfuko wa hifadhi ya jamii unao hudumia watumishi wa umma.
Naye mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Ifakara Mh Mashaka Mbilinyi amesema kuwa anatarajia kuona vikundi hivi vinaitumia fulsa hii muhimu ili waweze kunufaika na mafao yanayotolewa na mfuko huo kwa swala la afya ni muhimu sana ili waweze kutekeleza majukumu yao, pia ameomba agenda ya afya iwe inaingizwa katika kila kikao kutokana na umuhimu wake.
Kwa upande wa viongozi wa vikundi wameishukuru serikali na NSSF kwa kuwapa elimu na nafasi ya kujiunga na mfuko huo na kuahidi kuitumia fursa hii kwa kujiunga na kuhamasisha wanachama wa vikundi vyao kujiunga.
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: 0738 223 543
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa