Wananchi wa Halmashauri Mji Ifakara wameishukuru serikali kwa ujenzi wa barabara ya Keepleft Polisi {UPOGORO} kwa kiwango cha changalawe yenye urefu wa kilomita 1 point 3 ambayo ni kero kubwa hasa nyakati za masika.
Hayo yameelezwa na wananchi hao walipotembelewa na mwanahabari wetu katika ujenzi wa barabara hiyo inayejengwa na kampuni ya classic bulder general suppries, ambayo inaghalim shilingi 436 milioni.
Kwa upande wa menaja wa wakala wa barabara za mijini na vijijini [TARURA] Halmashauri Mji Ifakara Bw. Emmanuel Mfinanga amesema kuwa mradi huo unatarajiwa kukamilika kabla ya mwezi wa 11 mwaka huu.
Mfinanga pia amewaomba wananchi kuitunza barabara hiyo pindi itakapo kamilika na kuwahasa watumiaji wa barabara hasa waendesha vyombo vya moto kuwa makini wawapo barabarani ili kuepuka ajari za barabarani.
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: 0738 223 543
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa