Wamiliki na wasimamizi wa mashine pamoja na magala ya kuifadhia mpunga wa Halmashauri ya mji Ifakara wametakiwa kulipa ushuru kutokana na muongoza wa mwaka wa fedha 2017/18 kwani mojakwa moja wanahusika na ulipaji wa kodi hizo kulingana na biashara zao wanazo fanya kila siku.
Hayo yamesemwa na mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara Ndugu FRANCIS NDULANE wakati akiongea na wafanya biashara wa mashine pamoja na maghala katika kikao cha kwanza cha mabadiliko ya mwongozo wa tozo za kodi katika ukumbi wa chuo cha maendeleo mjini Ifakara.
Hata hivyo NDULANE amesema kuwa amefurahishwa kwa kuona wamiliki na wasimamizi wa biashaa hizo na si wawakilishi kwani moja kwa moja biashara yenu imekuwa kivutio cha watuwengi wakiita ifakara yetu kuwa ya mchele kwani mmeshilkilia katika maeneo muhimu zaidi.
Aidha Ndugu NDULANE amefurahishwa na ufanisi mkubwa wa ukusanywaji wa mapato unaofanywa na wafanya biashara wa mashine na maghala kwa kukusanya ushuru wa mpunga na ushuru wa kuifadhi mpunga kwa karibu95%kwani imeiyongezea Halmashauri kipato.
Pamoja na hayo amesema kuwa wafanya biahara hawa niwatu muhimu katika Halmashauri kwani kilimo nikichocheo kikubwa cha maendeleo na pia waendeleze juhudi za kuendelea kuchakata mpunga na kuwasaidia wakulima wetu kuwapatia mbegu bora ya mpunga.
Naye Afisa ushirika na masoko wa Halmashauri hiyo Malika Mabuba alifafanua sheria hiyo kwani imegusa maeneo manne ambayo ni ya ushuru wa mazao ya biashara na ushuru wa hoteli pamoja na ushuru wa mabongo ushuru huu utakuwa unakusanywa na mamlaka ya mapato Tanzania “TRA”hivyo mamlaka ya serikali za mitaa hazito kusanya ushuru wa bango na faini zitatozwa kwa watakao vunja sharia hiyo ambayo imeeleza kuwa ushuru wa mazao ya biashara uliokuwa ukitozwa kati ya 3% na 5% na sasa utatozwa kwa 3% pekee hukumazao ya chakula yakitozwa kwa 2% pekee
Mabuba ameongeza kuwa kwa sheria hiyo inataka mashine na maghala kulipia ushuru wa huduma ya mapato yako yote utakayo pata kama umeuza mazao au umepokea unapaswa kuondoa 0.3 ya mapato hayo na kuyalipai Halmashauri napia ilikuja kama utakacho kuwa unakipata niahalali inatupasa kutunza kumbukumbu pamoja na hayo ushuru huu unaweza kulipia hata kwa miezi 3 ,
Pia amesema kuwa katika kodi ya majengo kuna majengo ya mashine na ya maghala haya pia yanatakiwa kulipiwa kodi ya mapato kwani mapato hayo hayata kusanywa na Halmashauri wala serikali za mitaa itakusanywa na “TRA” hatahivyo imeainisha maeneo yatakayo lipia kodi Halmashauri ya wilaya itaanza kutoza kodi ya majengo miji midogo na makao makuu ya wilaya hata hivyo kodi hiyo haita tozwa maeneo ya vijijini bali mamlaka ya mapato itaendelea kukusanya katika maeneo ya majiji na manispaa.
Azabu zilizo kuwa zimewekwa awali ilikuwa nifaini ya 50,000 na azabu ya kifungo kwa miezi 12 lakini kwa mwaka wa fedha 2017/18 imebadilisha kutoka 200,000/= na kisicho zidi 1,000,000/= na kifungo kisicho pungua mwaka 1,na kisicho zidi miaka 2 au adhabu zote mbili kwa pamoja .Aliongeza MABUBA.
Kwaupande wake mtunza hazina HAIRE NJITANGO ameongeza kuwa mapato haya yanalengo la kutoa huduma mbalimbali ikiwemo Elimu , huduma ya maji ,Afya pamoja na kuboresha miundo mbinu ya barabara na utatozwa kutokana na ukubwa wa biashara yako naili tuweze kufikia malengo yetu sheria inaelekeza kutokudanganya katika ulipaji wa kodi ili tuweze kufikia wa kati .
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: 0738 223 543
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa