Shukrani hizo zimetolewa katika Hafla fupi iliyoandaliwa na Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara na kufanyika leo Januari 12,2024 Ukumbi wa Mazingira Mjini Ifakara.
Mgeni rasmi ambae ni Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Mhe. Dunstan Kyobya ametoa vyeti maalum vinavyoonesha kuthaminiwa kwa mchango wao.
"Ushindi wetu ni wa pamoja hivyo sina budi kuwashukuru na Kwa kufanikisha matokeo mazuri tuliyoyapata Mwaka 2023". Amesema DC Kyobya
Sambamba na hayo DC Kyobya ameeleza bayana kuwa ushindi wa Mwaka Jana umetokana na uongozi imara toka kwa Mkurugenzi aliyepita Lena Nkaya na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Ifakara Mhe.Kassim Nakapala.
Viongozi mbalimbali kutoka Vyama vya Siasa, Taasisi za Serikali, Wafanyabiashara,Vyama vya Wafanyakazi na wengine wamehudhuria hafla hiyo.
Ikumbukwe kuwa matokeo ya Mwenge Mwaka 2023, Halmashauri ya Mji Ifakara ilishinda nafasi zifuatazo; ya 2 kimkoa,13 kikanda na 40 kitaifa.
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: -
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa