• Nukuu ya Ukaribisho
  • Maswali ya mara kwa mara
  • Mawasiliano Yetu
Ifakara Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
Halmashauri ya Mji Ifakara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dira na Dhamira
    • Historia
    • Taswira
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Biashara
    • Ukaguzi wa Ndani
    • Manunuzi & Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Ustawi wa Jamii
    • TEHAMA
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Hatua
    • Ripoti
  • Uwekezaji
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Kapu
    • Utamaduni,Sanaa & Michezo
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Videos

ZIARA YA KAMATI YA BUNGE YA VIWANDA, BIASHARA, KILIMO NA MIFUGO.

Posted on: February 19th, 2025

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo, ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Deodatus Philip Mwanyika (Mb), imefanya ziara yake katika Miradi mbalimbali inayopatikana Halmashauri ya Mji Ifakara, Wilayani Kilombero ambapo baadhi ya Miradi hiyo ni Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Tanzania (TARI) Ifakara, Ifakara White Rice Milling machines, pamoja na kiwanda cha Sukari Kilombero (K4) Februari 19, 2025.


TARI Ifakara  kinajishughulisha na utafiti wa mazao mbalimbali, hususan mpunga, kwa lengo la kuboresha,uzalishaji na tija kwa wakulima pia kuweza kuja na mbegu bora zitakazo vumilia mafuriko.


Katika ziara hiyo, kamati imelenga kujionea shughuli za utafiti na maendeleo ya kilimo zinazofanywa katika kituo cha TARI Ifakara pia ilipata fursa ya kutembelea maabara za utafiti, shamba darasa, na maeneo mengine ya kituo, ambapo walijionea teknolojia na mbinu bunifu zinazotumika kuboresha kilimo.


Mhe. Mwanyika amezipongeza juhudi za TARI Ifakara katika kuendeleza sekta ya kilimo na kuhimiza ushirikiano zaidi kati ya kituo hicho na wadau mbalimbali ili kuhakikisha matokeo ya utafiti yanafikia wakulima kwa ufanisi na kuahidi kuja na namna bora ya kuongeza wafanyakazi ambao watakuwa wanawafikia wakulima moja Kwa moja.


Ziara hii inaendana na mikakati ya serikali ya kuinua sekta ya kilimo kupitia uwekezaji katika utafiti na maendeleo, ili kuongeza uzalishaji na kuinua kipato cha wakulima Halmashauri ya Mji Ifakara na nchini Kwa ujumla.


Mhe.David Silinde Naibu waziri wa Kilimo amesema wanaifakara wajifunze kuwekeza katika viwanda kwani serikali ipo tayari kuwaunga Mkono wananchi wote wenye nia ya kuwekeza kupitia Mfuko wa pembejeo (AGITF)ambao unajihusisha na utoaji wa  Mikopo Kwa wakulima kwenye mnyororo wa kuongeza thamani.


Hata hivyo Kwa upande wake Mhe.Ng'wasi Kamani  Mbunge Muwakilishi Vijana Taifa amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imelenga kunyanyua watanzania wote kwani wamejionea uwekezaji mkubwa katika sekta  ya kilimo.





Latest Announcements

  • TANGAZO LA MAOMBI YA MPIGA KURA KUPIGA KURA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KATIKA KITUO TOFAUTI NA KITUO ALICHOJIANDIKISHA

    read more
  • TANGAZO LA ULIPAJI WA ADA NA USHURU KWA WANANCHI, WAFANYABIASHARA NA TAASISI MBALIMBALI IFAKARA MJI

    read more
  • View More

Habari Mpya

  • BENKI YA CRDB YAKABIDHI VITI NA MEZA 100 SHULE YA SEKONDARI MAHUTANGA
  • CHUO KIKUU CHA SOKOINE CHA KILIMO (SUA) KUWEZESHA VIJANA KUONGEZA UZALISHAJI NA MNYORORO WA THAMANI WA MAZAO - HALMASHAURI YA MJI IFAKARA
  • KAMATI YA USALAMA YA WILAYA YA KILOMBERO (KU) YAMPONGEZA MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MJI IFAKARA BI . PILLY KITWANA KWA USIMAMIZI MZURI WA MIRADI YA MAENDELEO
  • WAZEE WATAKIWA KUENDELEA KUDUMISHA AMANI NCHINI
  • WADAU WA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI WATAKIWA KUWASAIDIA WANANCHI KUPATA MBEGU BORA
  • More

Mawasiliano Yetu

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji Ifakara
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Simu ya Mkononi: -

Kurasa za Haraka

  • CHF
  • Ramani ya halmashauri ya mji wa Ifakara
  • MATOKEO KIDATO CHA NNE 2024
  • BOFYA HAPA KUOMBA KITAMBULISHO CHA WAJASILIAMALI WADOGO
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2024

Kurasa Mfanano

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Wizara ya Tamisemi
  • Wizara ya utumishi wa uma
  • Tovuti ya mkoa wa Morogoro
  • Tovuti ya Ajira Tanzania

Mitandao ya Kijamii

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya Uhifadhi
  • Maswali ya mara kwa mara
  • Ramani