KAYA MASKINI ZILIZO TAMBULIWA ZAINGIZWA KWENYE MFUMO ILI KUWEZESHA SERIKALI KUTOA HUDUMA KWA HARAKA NA KWA UFANISI
KAYA MASKINI ZILIZO TAMBULIWA KUPITIA MIKUTANO YA WANANCHI ZAINGIZWA KWENYE MFUMO ILI KUWEZESHA SERIKALI KUTOA HUDUMA KWA HARAKA NA KWA UFANISI
Na: Jacqueline Jerome -IfakaraTC, Habari
TASAF Kwa kushirikiana na Halmashauri ya Mji Ifakara imefanikiwa kuingiza kwenye mfumo Kaya maskini zilizotambuliwa kupitia mikutano ya hadhara iliyofanyika katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri ya Mji Ifakara ikiwa ni hatua muhimu ya kuboresha daftari la Walengwa,ukusanyaji na usimamizi wa taarifa za kijamii.
Utambuzi huo umefanyika kwa kushirikisha wananchi ili kuhakikisha Kaya zenye hali duni zinabainika kwa uwazi na haki, kulingana na vigezo vilivyowekwa.
Uingizaji wa taarifa hizo kwenye mfumo unalenga kuwezesha Serikali kupata takwimu sahihi na halisi zitakazosaidia katika kupanga na kutoa huduma za kijamii kwa ufanisi zaidi. Kupitia mfumo huo, Serikali itaweza kuchukua hatua za haraka hususan pale majanga ya asili yatakapojitokeza, kwa kuwafikia Walengwa kwa wakati kulingana na mipango itakayowekwa.
Aidha, hatua hiyo itasaidia kurahisisha utekelezaji wa mipango ya kupunguza umaskini, kuboresha maisha ya wananchi na kuhakikisha rasilimali za Serikali zinawafikia walengwa waliokusudiwa.
Taarifa za kaya zilizotambuliwa zitasaidia Serikali katika utekelezaji wa Programu mbalimbali za Kiuchumi na Kijamii kwa maslahi mapanaa ya Wananchi.
Wananchi wametakiwa kuendelea kushirikiana na viongozi pamoja na Wataalamu wakati wa zoezi hilo ili taarifa zinazokusanywa ziwe sahihi na zenye manufaa kwa maendeleo ya jamii kwa ujumla