MADIWANI WILAYA YA KILOMBERO WATAKIWA KUIBUA NA KUSIMAMIA MIRADI YA MAENDELEO KATIKA KATA
MADIWANI WILAYA YA KILOMBERO WATAKIWA KUIBUA NA KUSIMAMIA MIRADI YA MAENDELEO KATIKA KATA ZAO
Na: Nuru Mangalili- Ifakara TC ,Habari
Hayo yamesemwa Jumanne tarehe 6 /1/2026 na Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Mhe. Wakili Dunstan Kyobya wakati akifungua Mafunzo Elekezi ya Kuwajengea uwezo Madiwani wa Wilaya ya Kilombero Halmashauri ya Mji Ifakara na Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba yanayofanyika Katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mlimba uliopo Ifakara .
Mhe. Kyobya aliwataka kila Diwani katika Kata yake ahakikishe anakwenda kusimamia Miradi ya Maendeleo, Mapato, Mikopo ya Asilimia Kumi, Uhifadhi wa Mazingira, Vyanzo vya Maji, Kutatua Kero za Wananchi,Miundo Mbinu ya Barabara, Mirathi , Maadili na Talaka , ulinzi na usalama katika Maeneo yao Ili kuhakikisha Wilaya ya Kilombero inasonga Mbele na kuleta tabasamu kwa Wananchi wa Kilombero kama ilivyo adhma ya Mhe . Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhakikisha kila mwananchi anapata tabasamu .
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara Bi. Pilly Kitwana aliwapongeza Waheshimiwa Madiwani kwa Mafunzo hayo na kuahidi kuwapa Ushirikiano katika Utekelezaji wa Majukumu yao ya kila siku Ili kuhakikisha Halmashauri ya Mji Ifakara inasonga Mbele na Kero za Wananchi kutatuliwa kwa wakati .
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba Mhe. Martha Daniel Mkula alishukuru kwa Mafunzo madiwani na kuahidi kwenda Kutekeleza kwa Ufanisi Yale yote watakayofundishwa na kuhakikisha wanakwenda kubuni miradi mipya na inatekelezeka kwa wakati.
Aidha Mafunzo hayo yalihudhuriwa na Katibu Tawala Msaidizi anayeshughulikia Masuala ya Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro Bi. Neema Dachi na Bw. Lucas Charles Malunde kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu - OWM - TAMISEMI ambapo waliwasisitiza Madiwani hao Kuzingatia mada wanazofundishwa katika Mafunzo hayo Ili zikalete Ufanisi katika Utendaji wao.
Mafunzo hayo ya siku tatu yalianza tarehe 5 Januari 2026 na yanatarajiwa kuhitimishwa tarehe 7 Januari 2025 . Mafunzo hayo yanatolewa na Wakufunzi kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo.