• Nukuu ya Ukaribisho
  • Maswali ya mara kwa mara
  • Mawasiliano Yetu
Ifakara Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
Halmashauri ya Mji Ifakara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dira na Dhamira
    • Historia
    • Taswira
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Biashara
    • Ukaguzi wa Ndani
    • Manunuzi & Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Ustawi wa Jamii
    • TEHAMA
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Hatua
    • Ripoti
  • Uwekezaji
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Kapu
    • Utamaduni,Sanaa & Michezo
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Videos

ZIARA YA CMT KUTEMBELEA MIRADI YA MAENDELEO TAREHE 18 /9/2025

Posted on: September 19th, 2025

MENEJIMENTI YA HALMASHAURI YA MJI IFAKARA YAFANYA ZIARA KUTEMBELEA MIRADI YA MAENDELEO

Timu ya Menejimenti ya Halmashauri ya Mji Ifakara imefanya Ziara ya kutembelea Miradi Mbalimbali ya Maendeleo inayotekelezwa na Halmashauri ya Mji Ifakara. Ziara hiyo imefanyika siku ya Alhamisi tarehe 18 Septemba 2025 ambapo iliongozwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara akiambatana na Katibu Tawala wa Wilaya ya Kilombero Bw. Abraham Mwaikwila.


Miradi iliyotembelewa ni pamoja na Miradi iliyoletewa Fedha na Serikali zaidi ya Milioni 892.3 kwa mwaka wa Fedha 2024 -2025 kupitia BOOST na GPE LANES kwaajili ya Ujenzi wa Miradi Mipya ya Elimu ya Awali na Msingi ndani ya Halmashauri ya Mji Ifakara ikiwemo Ujenzi wa Shule Mpya, Madarasa , vyoo , nyumba za Walimu na Ujenzi wa Kituo cha Walimu (TRC) Mkamba na pia walitembelea  Umaliziaji wa Jengo la Maabara  OPD na Kichomea Taka katika Hospitali ya Halmashauri ya Mji Ifakara iliyopo Kiberege wenye thamani ya Shilingi Milioni 65,000,000/= na pia walitembelea kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Jengo la Utawala.


Akizungumza katika Ziara hiyo Katibu Tawala wa Wilaya ya Kilombero Bw. Abraham Mwaikwila alipongeza hatua mbalimbali zilizofikiwa katika ukamilishaji wa Miradi hiyo na kusisitiza kuongezeka  kwa kasi ya utekelezaji ili kuendana na muda uliopangwa ili miradi hiyo iweze kuwasaidia wananchi wa Ifakara hususani katika kupunguza adha ya umbali mrefu kwa wanafunzi kufuata masomo na pia kuongeza ukaribu wa upatikanaji wa Huduma za Afya kwa Wakati.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara Bi. Pilly Kitwana aliwasisitiza wasimamizi wa Miradi hiyo kuhakikisha Vifaa vinapatikana muda wote katika maeneo yote ya miradi na pia kuhakikisha miongozo , taratibu na kanuni zinafuatwa . Aidha alisisitiza kuongezeka kwa kasi ya ukamilishaji wa Miradi hiyo kulingana na hali ya hewa hususani katika hiki kipindi ambacho Mvua zinatarajiwa kuanza wakati wowote.

Latest Announcements

  • TANGAZO LA MAOMBI YA MPIGA KURA KUPIGA KURA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KATIKA KITUO TOFAUTI NA KITUO ALICHOJIANDIKISHA

    read more
  • TANGAZO LA ULIPAJI WA ADA NA USHURU KWA WANANCHI, WAFANYABIASHARA NA TAASISI MBALIMBALI IFAKARA MJI

    read more
  • View More

Habari Mpya

  • MAANDALIZI YA MPANGO MKAKATI WA HALMASHAURI KWA MWAKA 2026/27 HADI 20230/31
  • MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MJI IFAKARA, TIMU YA MENEJIMENTI WAPONGEZWA
  • MHESHIMIWA KASSIM FAYA NAKAPALA ASHINDA NAFASI YA MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA MJI IFAKARA
  • MHESHIMIWA KASSIM FAYA NAKAPALA ASHINDA NAFASI YA MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA MJI IFAKARA
  • KATIBU WA CHAMA CHA MAPINDUZI WILAYA YA KILOMBERO AWATAKA MADIWANI KUHAKIKISHA KERO ZA WANANCHI ZINATATULIWA
  • More

Mawasiliano Yetu

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji Ifakara
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Simu ya Mkononi: -

Kurasa za Haraka

  • CHF
  • Ramani ya halmashauri ya mji wa Ifakara
  • MATOKEO KIDATO CHA NNE 2024
  • BOFYA HAPA KUOMBA KITAMBULISHO CHA WAJASILIAMALI WADOGO
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2024

Kurasa Mfanano

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Wizara ya Tamisemi
  • Wizara ya utumishi wa uma
  • Tovuti ya mkoa wa Morogoro
  • Tovuti ya Ajira Tanzania

Mitandao ya Kijamii

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya Uhifadhi
  • Maswali ya mara kwa mara
  • Ramani