• Nukuu ya Ukaribisho
  • Maswali ya mara kwa mara
  • Mawasiliano Yetu
Ifakara Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
Halmashauri ya Mji Ifakara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dira na Dhamira
    • Historia
    • Taswira
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Biashara
    • Ukaguzi wa Ndani
    • Manunuzi & Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Ustawi wa Jamii
    • TEHAMA
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Hatua
    • Ripoti
  • Uwekezaji
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Kapu
    • Utamaduni,Sanaa & Michezo
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Videos

WILAYA YA KILOMBERO YAZINDUA MAADHIMISHO YA WIKI YA SHERIA 2025

Posted on: January 25th, 2025

Wilaya ya Kilombero Januari 25,2025 imezindua Maadhimisho ya Wiki ya Sheria nchini  katika Viwanja vya Mahakama ya Wilaya ya Kilombero iliyopo Halmashauri ya Mji Ifakara .

Uzinduzi huo ulitanguliwa na maandamano yaliyoanzia Stendi Kuu ya Mabasi Kibaoni mpaka Mahakama ya Wilaya ya Kilombero ambapo Mgeni Rasmi katika Uzinduzi huo alikua Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Mhe. Wakili Dunstan Kyobya ambaye aliwataka Wananchi wa Wilaya hiyo kujitokeza kwa wingi kupata huduma za Kisheria katika maeneo na vituo mbalimbali vilivyowekwa kutoa huduma hizo ili wapate ufumbuzi na  utatuzi wa Migogoro mbalimbali ya Kisheria.

"Kuna migogoro tofautitofauti ya  Ardhi, mirathi, talaka n.k hivyo taasisi zinazohusika na haki jinai wahakikishe watu wanapata haki zao katika jamii". alisisitiza Mhe . Kyobya

Kwa upande wake Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Kilombero ,Mhe. Regina Futakamba aliwasisitiza Wananchi wa Kilombero kujitokeza kupata huduma hizo ikiwemo Elimu na utatuzi wa Migogoro ya Kisheria.

" Huduma hii imezinduliwa leo 25 /1/2025 hadi tarehe 1/2/2025 na kilele chake itakua tarehe 3/2/2025 hivyo ni vyema Wananchi kutumia fursa hii katika Vituo vinavyotoa Elimu za Kisheria na huduma hii inatolewa buree". Alieleza Mhe. Regina

Aidha Mhe. Regina alivitaja Vituo vinavyotoa huduma hizo za Sheria kuwa ni Stendi ya Kibaoni, Mahakama ya Wilaya na Mahakama zote za Mwanzo.

Kauli mbiu katika Maadhimisho hayo ya Wiki ya Sheria ni " Tanzania ya  2050: Nafasi ya Taasisi zinazo Simamia haki Madai katika Kufikia Malengo Makuu ya Dira ya Taifa ya Maendeleo".









Latest Announcements

  • TANGAZO LA MAOMBI YA MPIGA KURA KUPIGA KURA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KATIKA KITUO TOFAUTI NA KITUO ALICHOJIANDIKISHA

    read more
  • TANGAZO LA ULIPAJI WA ADA NA USHURU KWA WANANCHI, WAFANYABIASHARA NA TAASISI MBALIMBALI IFAKARA MJI

    read more
  • View More

Habari Mpya

  • BENKI YA CRDB YAKABIDHI VITI NA MEZA 100 SHULE YA SEKONDARI MAHUTANGA
  • CHUO KIKUU CHA SOKOINE CHA KILIMO (SUA) KUWEZESHA VIJANA KUONGEZA UZALISHAJI NA MNYORORO WA THAMANI WA MAZAO - HALMASHAURI YA MJI IFAKARA
  • KAMATI YA USALAMA YA WILAYA YA KILOMBERO (KU) YAMPONGEZA MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MJI IFAKARA BI . PILLY KITWANA KWA USIMAMIZI MZURI WA MIRADI YA MAENDELEO
  • WAZEE WATAKIWA KUENDELEA KUDUMISHA AMANI NCHINI
  • WADAU WA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI WATAKIWA KUWASAIDIA WANANCHI KUPATA MBEGU BORA
  • More

Mawasiliano Yetu

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji Ifakara
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Simu ya Mkononi: -

Kurasa za Haraka

  • CHF
  • Ramani ya halmashauri ya mji wa Ifakara
  • MATOKEO KIDATO CHA NNE 2024
  • BOFYA HAPA KUOMBA KITAMBULISHO CHA WAJASILIAMALI WADOGO
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2024

Kurasa Mfanano

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Wizara ya Tamisemi
  • Wizara ya utumishi wa uma
  • Tovuti ya mkoa wa Morogoro
  • Tovuti ya Ajira Tanzania

Mitandao ya Kijamii

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya Uhifadhi
  • Maswali ya mara kwa mara
  • Ramani