• Nukuu ya Ukaribisho
  • Maswali ya mara kwa mara
  • Mawasiliano Yetu
Ifakara Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
Halmashauri ya Mji Ifakara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dira na Dhamira
    • Historia
    • Taswira
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Biashara
    • Ukaguzi wa Ndani
    • Manunuzi & Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Ustawi wa Jamii
    • TEHAMA
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Hatua
    • Ripoti
  • Uwekezaji
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Kapu
    • Utamaduni,Sanaa & Michezo
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Videos

WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA WATAKIWA KUWA MSTARI WA MBELE KATIKA KUTATUA KERO ZA WANANCHI

Posted on: January 7th, 2025

Wenyeviti wa Vitongoji, Vijiji na Mitaa wa Halmashauri ya Mji Ifakara wametakiwa kuhakikisha wanasikiliza na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wananchi katika maeneo yao.


Hayo yamesemwa   Januari 7 ,2024 na Afisa Tawala wa Wilaya ya Kilombero Phabius Byamungu alipokua akimuwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Mhe. Wakili Dunstan Kyobya aliyekuwa Mgeni Rasmi wakati wa   kufungua Mafunzo Elekezi kwa  Wenyeviti wa Mitaa, Vitongoji na Vijiji katika Ukumbi wa Mlimba uliopo Halmashauri ya Mji Ifakara.


Aidha aliwataka  Wenyeviti hao  kuhakikisha wanasimamia suala la Ulinzi na usalama katika maeneo yao, kupambana na Rushwa, kupinga ukatili wa kijinsia, kusimamia Mazingira, kushiriki katika miradi ya Maendeleo na kuibua vyanzo vya mapato.


" Twende tukatende haki tukawasikilize Wananchi wetu, tukasimamie majukumu yetu,tunatarajia ninyi ndio muwe mfano na walimu mara baada ya Mafunzo haya". Alieleza Bw .Byamungu


Mmoja wa  Wenyeviti hao Bw. Geoffrey Mtapika ambaye ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Njokamoni  Kata ya Mang' ula aliishukuru  Halmashauri ya Mji Ifakara kwa  kuwapatia Mafunzo hayo kwani yatakua muongozo katika majukumu yao na kuahidi kuboresha maeneo yote yaliyokua na mapungufu .


"Ninashukuru kwa Mafunzo haya kwani yananipa mwanga katika Shughuli zangu za kiutendaji".Alisema Bw. Geofrey.


Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu wa Halmashauri ya Mji Ifakara Bw. Rashid Semngoya alisema Mafunzo hayo yameandaliwa kwa Viongozi hao Ili waweze kutambua majukumu yao na kufanya Kazi kwa ufanisi. Aidha Mafunzo hayo yalitolewa na  wawezeshaji  kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa  (LGTI) - Hombolo .





Latest Announcements

  • TANGAZO LA MAOMBI YA MPIGA KURA KUPIGA KURA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KATIKA KITUO TOFAUTI NA KITUO ALICHOJIANDIKISHA

    read more
  • TANGAZO LA ULIPAJI WA ADA NA USHURU KWA WANANCHI, WAFANYABIASHARA NA TAASISI MBALIMBALI IFAKARA MJI

    read more
  • View More

Habari Mpya

  • MAANDALIZI YA MPANGO MKAKATI WA HALMASHAURI KWA MWAKA 2026/27 HADI 20230/31
  • MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MJI IFAKARA, TIMU YA MENEJIMENTI WAPONGEZWA
  • MHESHIMIWA KASSIM FAYA NAKAPALA ASHINDA NAFASI YA MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA MJI IFAKARA
  • MHESHIMIWA KASSIM FAYA NAKAPALA ASHINDA NAFASI YA MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA MJI IFAKARA
  • KATIBU WA CHAMA CHA MAPINDUZI WILAYA YA KILOMBERO AWATAKA MADIWANI KUHAKIKISHA KERO ZA WANANCHI ZINATATULIWA
  • More

Mawasiliano Yetu

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji Ifakara
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Simu ya Mkononi: -

Kurasa za Haraka

  • CHF
  • Ramani ya halmashauri ya mji wa Ifakara
  • MATOKEO KIDATO CHA NNE 2024
  • BOFYA HAPA KUOMBA KITAMBULISHO CHA WAJASILIAMALI WADOGO
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2024

Kurasa Mfanano

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Wizara ya Tamisemi
  • Wizara ya utumishi wa uma
  • Tovuti ya mkoa wa Morogoro
  • Tovuti ya Ajira Tanzania

Mitandao ya Kijamii

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya Uhifadhi
  • Maswali ya mara kwa mara
  • Ramani