• Nukuu ya Ukaribisho
  • Maswali ya mara kwa mara
  • Mawasiliano Yetu
Ifakara Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
Halmashauri ya Mji Ifakara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dira na Dhamira
    • Historia
    • Taswira
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Biashara
    • Ukaguzi wa Ndani
    • Manunuzi & Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Ustawi wa Jamii
    • TEHAMA
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Hatua
    • Ripoti
  • Uwekezaji
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Kapu
    • Utamaduni,Sanaa & Michezo
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Videos

WAZEE WATAKIWA KUENDELEA KUDUMISHA AMANI NCHINI

Posted on: October 1st, 2025

WAZEE WATAKIWA KUENDELEA KUDUMISHA AMANI NCHINI 

Wazee wa Halmashauri ya Mji Ifakara wametakiwa kuendelea  kudumisha amani nchini haswa katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu tarehe 29 Oktoba 2025 na kushiriki kutumia haki yao ya Msingi kwa  kupiga Kura .

Rai hiyo imetolewa tarehe 1 Oktoba 2025 na Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Mhe. Wakili Dunstan Kyobya wakati alipokuwa Mgeni Rasmi kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani yaliyofanyika katika Kijiji cha Kilama Kata ya Kibaoni, Halmashauri ya Mji Ifakara.

Aidha katika Maadhimisho hayo Mhe. Kyobya  alisisitiza Jamii kuendelea kuwathamini Wazee na kuhakikisha wanapata haki zao za Msingi ikiwemo  kupewa fursa ya kupata  Mikopo ya Asilimia 10 na WBN.

“Maafisa Maendeleo ya Jamii hakikisheni Wazee wanapata Mikopo, umri wa Kijana umeongezeka kutoka Miaka 35 hadi 40 na kwa upande wa wanawake na watu wenye ulemavu umri hauna mwisho ili mradi ukidhi masharti ya Mikopo hiyo”. Alieleza Mhe. Kyobya.

Awali Wazee hao katika Risala yao walieleza Changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwemo changamoto za Afya, Migogoro ya Ardhi, Saikolojia, Sheria n.k

Wakati huo huo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara Bi. Pilly Kitwana alisema kuwa Halmashauri imepokea changamoto za Wazee hao na kuahidi  kuzifanyia kazi kwa haraka,baadhi ikiwemo changamoto za Bima ya Afya, Dawa n.k . Aidha alieleza kuwa baadhi ya Changamoto zimeshaanza kutatuliwa ikiwemo utoaji wa Kadi za Bima za Afya za CHF kwa wazee 300 na Wajane 300.

Aidha,  takwimu zinaonesha Jumla ya Wazee Elfu 21, 468 wapo ndani ya Halmashauri ya Mji Ifakara kwa Kata zote 19 wakiwemo Wanaume 9611 na Wanawake 11857.

Kauli Mbiu katika Maadhimisho hayo kwa mwaka huu ilikuwa ni “Wazee Tushiriki Uchaguzi kwa Ustawi wa Jamii Yetu”.

Latest Announcements

  • TANGAZO LA MAOMBI YA MPIGA KURA KUPIGA KURA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KATIKA KITUO TOFAUTI NA KITUO ALICHOJIANDIKISHA

    read more
  • TANGAZO LA ULIPAJI WA ADA NA USHURU KWA WANANCHI, WAFANYABIASHARA NA TAASISI MBALIMBALI IFAKARA MJI

    read more
  • View More

Habari Mpya

  • BENKI YA CRDB YAKABIDHI VITI NA MEZA 100 SHULE YA SEKONDARI MAHUTANGA
  • CHUO KIKUU CHA SOKOINE CHA KILIMO (SUA) KUWEZESHA VIJANA KUONGEZA UZALISHAJI NA MNYORORO WA THAMANI WA MAZAO - HALMASHAURI YA MJI IFAKARA
  • KAMATI YA USALAMA YA WILAYA YA KILOMBERO (KU) YAMPONGEZA MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MJI IFAKARA BI . PILLY KITWANA KWA USIMAMIZI MZURI WA MIRADI YA MAENDELEO
  • WAZEE WATAKIWA KUENDELEA KUDUMISHA AMANI NCHINI
  • WADAU WA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI WATAKIWA KUWASAIDIA WANANCHI KUPATA MBEGU BORA
  • More

Mawasiliano Yetu

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji Ifakara
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Simu ya Mkononi: -

Kurasa za Haraka

  • CHF
  • Ramani ya halmashauri ya mji wa Ifakara
  • MATOKEO KIDATO CHA NNE 2024
  • BOFYA HAPA KUOMBA KITAMBULISHO CHA WAJASILIAMALI WADOGO
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2024

Kurasa Mfanano

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Wizara ya Tamisemi
  • Wizara ya utumishi wa uma
  • Tovuti ya mkoa wa Morogoro
  • Tovuti ya Ajira Tanzania

Mitandao ya Kijamii

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya Uhifadhi
  • Maswali ya mara kwa mara
  • Ramani