• Nukuu ya Ukaribisho
  • Maswali ya mara kwa mara
  • Mawasiliano Yetu
Ifakara Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
Halmashauri ya Mji Ifakara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dira na Dhamira
    • Historia
    • Taswira
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Biashara
    • Ukaguzi wa Ndani
    • Manunuzi & Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Ustawi wa Jamii
    • TEHAMA
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Hatua
    • Ripoti
  • Uwekezaji
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Kapu
    • Utamaduni,Sanaa & Michezo
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Videos

WATUMISHI HALMASHAURI YA MJI IFAKARA NA HALAMSAHURI YA WILAYA MLIMBA WAJENGEWA UWEZO JUU YA UTEKELEZAJI WA MFUMO WA USIMAMIZI WA UTENDAJI KAZI KATIKA UTUMISHI WA UMMA (e -UTENDAJI).

Posted on: June 26th, 2025


Na: Nuru Mangalili – Ifakara Tc , Habari

Wataalam Wilaya ya Kilombero wapatiwa mafunzo ya kuwajengea  uwezo juu ya Utekelezaji wa Mfumo wa Usimamizi wa Utendaji kazi katika Utumishi wa UMMA (e - Utendaji) leo Alhamisi tarehe 26 Juni 2025 katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mlimba uliopo Ifakara Mji. Wawezeshaji  katika Kikao hicho ni Bi. Shomi Jonas na Bw.  Mutani Josephat Manyama kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Aidha, Mafunzo hayo yamehudhuriwa na Wakurugenzi wa Halmashauri za Mji Ifakara na Halmashauri ya Wilaya Mlimba, Wakuu wa Idara, Vitengo, na Sehemu. Wafawidhi wa Vituo vya kutolea huduma za Afya, Maafisa Elimu Kata na Watendaji wa Kata wa Halmashauri zote mbili ambazo ni Halmashauri ya Mji Ifakara na Halmashauri ya Wilaya Mlimba.

Akizungumza wakati akihitimisha Mafunzo hayo Katibu Tawala wa Wilaya ya Kilombero Ndugu Abraham Mwaikwila aliwashukuru Wawezeshaji hao kwa kuwasaidia watumishi kuendelea kuuelewa Mfumo huo wa kupima utendaji kazi na shughuli zinazofanyika kila siku za Mtumishi kwa njia ya Mtandao.

“Kadri tunavyozidi kuutumia Mfumo  huu ndivyo tunavyozidi kuuelewa zaidi, Kikao hiki kimeendelea kutusaidia zaidi namna ya kutumia mfumo huu Vizuri tunawashukuru kwa mafunzo”. Alieleza Ndugu, Mwaikwila.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara Bw. Thomas Luambano alitoa Rai kwa kila Mtumishi kuhakikisha anafuatilia Mpango Mkakati na Malengo yake katika Mfumo huo wa Utendaji Kazi kwa Watumishi ili waweze kutumia Mfumo huo kwa wepesi


Wakati huohuo  Mkuu wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa  Rasilimali Watu Bw. Rashidi Semngoya  aliendelea kusisitiza watumishi kujaza majukumu yao ya kila siku katika Mfumo  huo 

”Mfumo huo utaamua utendaji kazi wa Mtumishi kama Mtu hatajaza majukumu yake ya kila siku mfumo unaweza kusababisha watumishi kutokwenda likizo, kukosa Mshahara, kutokupanda Vyeo, kushindwa kupata Mkopo n.k hivyo kila mtumishi ahakikishe anajaza na kutuma kwa Mkuu wake wa Idara, Kitengo na Sehemu na sisi Viongozi tunatakiwa tuhakikishe tuna idhinisha  kazi za Watumishi  na kuwafanyia tathmini .”. Alisisitiza Bw. Semgoya

Aidha, mmoja kati ya Wakufunzi hao kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw.  Mutani Manyama alisisitiza Viongozi kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa kuwafanyia tahmini watumishi kwenye Mfumo kwani wasipofanya hivyo Serikali itakosa taarifa za Mtumishi kwenye Mfumo .

Latest Announcements

  • TANGAZO LA MAOMBI YA MPIGA KURA KUPIGA KURA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KATIKA KITUO TOFAUTI NA KITUO ALICHOJIANDIKISHA

    read more
  • TANGAZO LA ULIPAJI WA ADA NA USHURU KWA WANANCHI, WAFANYABIASHARA NA TAASISI MBALIMBALI IFAKARA MJI

    read more
  • View More

Habari Mpya

  • BENKI YA CRDB YAKABIDHI VITI NA MEZA 100 SHULE YA SEKONDARI MAHUTANGA
  • CHUO KIKUU CHA SOKOINE CHA KILIMO (SUA) KUWEZESHA VIJANA KUONGEZA UZALISHAJI NA MNYORORO WA THAMANI WA MAZAO - HALMASHAURI YA MJI IFAKARA
  • KAMATI YA USALAMA YA WILAYA YA KILOMBERO (KU) YAMPONGEZA MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MJI IFAKARA BI . PILLY KITWANA KWA USIMAMIZI MZURI WA MIRADI YA MAENDELEO
  • WAZEE WATAKIWA KUENDELEA KUDUMISHA AMANI NCHINI
  • WADAU WA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI WATAKIWA KUWASAIDIA WANANCHI KUPATA MBEGU BORA
  • More

Mawasiliano Yetu

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji Ifakara
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Simu ya Mkononi: -

Kurasa za Haraka

  • CHF
  • Ramani ya halmashauri ya mji wa Ifakara
  • MATOKEO KIDATO CHA NNE 2024
  • BOFYA HAPA KUOMBA KITAMBULISHO CHA WAJASILIAMALI WADOGO
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2024

Kurasa Mfanano

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Wizara ya Tamisemi
  • Wizara ya utumishi wa uma
  • Tovuti ya mkoa wa Morogoro
  • Tovuti ya Ajira Tanzania

Mitandao ya Kijamii

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya Uhifadhi
  • Maswali ya mara kwa mara
  • Ramani