• Nukuu ya Ukaribisho
  • Maswali ya mara kwa mara
  • Mawasiliano Yetu
Ifakara Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
Halmashauri ya Mji Ifakara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dira na Dhamira
    • Historia
    • Taswira
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Biashara
    • Ukaguzi wa Ndani
    • Manunuzi & Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Ustawi wa Jamii
    • TEHAMA
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Hatua
    • Ripoti
  • Uwekezaji
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Kapu
    • Utamaduni,Sanaa & Michezo
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Videos

WATENDAJI WA KATA 19 ZA HALMASHAURI YA MJI IFAKARA WAKABIDHIWA PIKIPIKI.

Posted on: November 16th, 2024

Watendaji wa Kata 19 za Halmashauri ya Mji Ifakara  wamekabidhiwa Pikipiki ikiwa ni njia ya kutatua changamoto ya usafiri iliyokua ikiwakabili watendaji hao  hasa  katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.


Hafla hiyo imefanyika  Jumamosi tarehe 16 Novemba 2024 katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mlimba uliopo Halmashauri ya Mji Ifakara.


Pikipiki hizo zilinunuliwa mara baada ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara  Bi . Zahara Michuzi kukataa kununuliwa gari kutoka kwenye  Fedha za mapato ya ndani kiasi cha Shilingi Milioni 186,000,0000 zilizokua zimetengwa kwaajili ya Ununuzi wa Gari la Mkurugenzi, Hivyo badala yake akaomba fedha hizo zielekezwe  kwenye matumizi ya ununuzi wa Pikipiki za watendaji wa Kata 19 za Halmashauri ya Mji Ifakara, na kiasi kinachobakia kielezwe kwenye shughuli nyingine za miradi mbali mbali ya Maendeleo.


Hivyo  kupitia  Vikao mbalimbali vya kisheria vya Halmashauri, CMT na Madiwani wa Halmashauri ya Mji Ifakara kwa pamoja waliridhia ombi hilo la  ununuzi wa Pikipiki 19  zenye thamani ya Shilingi Milioni 67,450,000 kwa ajili ya watendaji wa kata wote 19.


"Niliona Watendaji  wa Kata wakipata shida  ya usafiri  katika kufikia  maeneo mbalimbali katika Kata zao , na wakati mwingine kuchelewesha kuhudumia Wananchi kwa wakati na hata kushindwa kufikia  vyanzo vyao vya mapato kwa ukamilifu, hivyo naamini kwa usafiri huu utawasaidia kusimamia kazi zao na Kutatua kero mbalimbali za wananchi". Alisema Bi. Zahara


 Mtendaji wa Kata ya Mwaya Bw. Acley Mhenga alimshukuru  Mkurugenzi huyo kwa kuwatatulia changamoto hizo  na kuwasihi watendaji wenzake  kuzitunza na kuzitumia vizuri Pikipiki hizo ili ziwe chachu ya  kufanya Kazi kwa weledi na ufanisi zaidi.


Mgeni Rasmi katika hafla hiyo alikua Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Mhe. Wakili Danstan Kyobya ambaye alimpongeza sana Mkurugenzi kwa uthubutu huo wa kuwajali watendaji wenzake wa kada ya chini kwa kuwaondolea adha ya muda mrefu ya  kukosa usafiri, na kuwasihi kwenda kuzitumia Pikipiki hizo kwa Kazi za Serikali kwa kutatua changamoto na kero za Wananchi.









Latest Announcements

  • TANGAZO LA MAOMBI YA MPIGA KURA KUPIGA KURA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KATIKA KITUO TOFAUTI NA KITUO ALICHOJIANDIKISHA

    read more
  • TANGAZO LA ULIPAJI WA ADA NA USHURU KWA WANANCHI, WAFANYABIASHARA NA TAASISI MBALIMBALI IFAKARA MJI

    read more
  • View More

Habari Mpya

  • MAANDALIZI YA MPANGO MKAKATI WA HALMASHAURI KWA MWAKA 2026/27 HADI 20230/31
  • MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MJI IFAKARA, TIMU YA MENEJIMENTI WAPONGEZWA
  • MHESHIMIWA KASSIM FAYA NAKAPALA ASHINDA NAFASI YA MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA MJI IFAKARA
  • MHESHIMIWA KASSIM FAYA NAKAPALA ASHINDA NAFASI YA MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA MJI IFAKARA
  • KATIBU WA CHAMA CHA MAPINDUZI WILAYA YA KILOMBERO AWATAKA MADIWANI KUHAKIKISHA KERO ZA WANANCHI ZINATATULIWA
  • More

Mawasiliano Yetu

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji Ifakara
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Simu ya Mkononi: -

Kurasa za Haraka

  • CHF
  • Ramani ya halmashauri ya mji wa Ifakara
  • MATOKEO KIDATO CHA NNE 2024
  • BOFYA HAPA KUOMBA KITAMBULISHO CHA WAJASILIAMALI WADOGO
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2024

Kurasa Mfanano

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Wizara ya Tamisemi
  • Wizara ya utumishi wa uma
  • Tovuti ya mkoa wa Morogoro
  • Tovuti ya Ajira Tanzania

Mitandao ya Kijamii

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya Uhifadhi
  • Maswali ya mara kwa mara
  • Ramani