WANANCHI WA KIJIJI CHA KATURUKILA WAHAMASISHWA KUSHIRIKI UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA
Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Mhe. Wakili Dunstan Kyobya amewahimiza wananchi wa Kijiji cha Katurukila kilichopo Kata ya Mkula kujitokeza kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa siku ya Jumatano tarehe 27 Novemba 2024.
Hayo ameyasema leo tarehe 19 Novemba 2024 wakati akizindua Kampeni ya Upandaji wa Miti ya Shule ya Msingi Katurukila iliyopo Kata ya Mkula Halmashauri ya Mji Ifakara.
"Asitokee Mtu yoyote akaharibu amani yetu, tuzingatie Amani na wote tukashiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa tuchague viongozi watakaotuletea Maendeleo katika maeneo yetu ". Alisema Mhe. Kyobya na kusisitiza
"yoyote mwenye umri wa miaka 18 na amejiandikisha kwenye Daftari la Mkazi akapige kura". Alimaliza Mhe. Kyobya
Aidha Jumla ya Miti 600 inatarajiwa kupandwa katika Kampeni hiyo ya Upandaji miti ya Shule ya Sekondari Katurukila.





