WANA KILOMBERO MKASHIRIKI UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA
Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Mhe. Wakili Dunstan Kyobya amewahimiza Wananchi wa Kata ya Ifakara na Wilaya ya Kilombero kwa ujumla wenye sifa za kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, kushiriki Uchaguzi huo ifikapo tarehe 27 Novemba 2024.
Hayo ameyasema leo Novemba 5, 2024 wakati alipokua akitatua Mgogoro wa Ardhi katika Mtaa wa Kilosa Mangwale uliopo Kata ya Ifakara.
Aidha, aliwasihi Viongozi wa Dini na Viongozi wengine wote kukumbusha watu kushiriki Uchaguzi huo.
" Zimebaki siku 22 kufikia tarehe ya uchaguzi , hivyo kila mwananchi mwenye sifa ya Kupiga kura , ashiriki kuchagua viongozi watakaoleta Maendeleo". Alisema Mhe. Kyobya.
Pia Mhe. Kyobya aliwaeleza Wananchi hao kujiandaa kwa ajili ya Tamasha kubwa la Kilombero FeStival litakalofanyika kuanzia Tarehe 6 hadi 8 , Desemba 2024 ambapo lengo la Tamasha hilo ni kuitangaza Kilombero katika Nyanja mbalimbali za utalii, Kilimo, uchumi, Uvuvi na utamaduni.


