Wakulima wapikwa kuzalisha Mazao bora
Wakulima wa Mazao mbalimbali kutoka Halmashauri ya Mji Ifakara wamepewa Mafunzo ya namna ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa,kuzuia sumu kuvu na Matumizi ya zana za Kilimo na uchaguzi wa Mbegu bora leo Aprili 18,2024.
Mafunzo hayo yametolewa katika Ukumbi wa Vijana ambapo yanaendeshwa na kampuni ya New Holland Agriculture ambapo yamezinduliwa na Kaimu Mkuu wa Divisheni ya Kilimo, Mifugo na uvuvi wa Halmashauri ya Mji Ifakara,Saida Selemani.


Hata hivyo Mafunzo yataendelea hadi Tarehe 19/04/2024