• Nukuu ya Ukaribisho
  • Maswali ya mara kwa mara
  • Mawasiliano Yetu
Ifakara Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
Halmashauri ya Mji Ifakara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dira na Dhamira
    • Historia
    • Taswira
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Biashara
    • Ukaguzi wa Ndani
    • Manunuzi & Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Ustawi wa Jamii
    • TEHAMA
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Hatua
    • Ripoti
  • Uwekezaji
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Kapu
    • Utamaduni,Sanaa & Michezo
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Videos

WAKULIMA WA HALMASHAURI YA MJI IFAKARA WAHAKIKISHIWA KUENDELEA KUZALISHA MAZAO NA KUPATA FAIDA ZAIDI KUPITIA MFUMO WA STAKABADHI GHALANI

Posted on: June 11th, 2025

Wakulima wa Mazao katika Halmashauri ya Mji Ifakara wamehakikishiwa  kuendelea kuzalisha Mazao yao na kupata faida zaidi kwa kupitia mfumo wa Stakabadhi za Ghala.Hayo yamesemwa tarehe 11 Juni 2025 wakati wa Kikao cha Kujadili namna ya kusimamia Utekelezaji wa Mfumo wa Stakabadhi Ghalani kwa  Wakulima wa Mazao mbalimbali hususani katika kuelekea Msimu wa Ufuta, kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano uliopo katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kilombero.

Kikao hicho kiliongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Mhe. Wakili Dunstan Dominick Kyobya ambapo kilishirikisha Bodi ya Usimamzii wa Stakabadhi za Ghala kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara, Viongozi wa Mabenki, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara Bw. Said Majaliwa na Wataalamu kutoka Mkoa wa  Morogoro na Halmashauri ya Mji Ifakara.

Aidha Mkurugenzi wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala Ndugu , Asangye Bangu alisema Mfumo wa Stakabadhi za Ghala  upo kuhakikisha wakulima wa Mazao mbalimbali kama Ufuta, Kokoa n.k wanapata bei za ushindani zilizoko Sokoni.

"Mkoa wa Morogoro umefanya jitihada kubwa kuhakikisha Mfumo wa Stakabadhi unafanya vizuri  hususani hapa Halmashauri ya Mji Ifakara, ambapo wakulima wataendelea kuzalisha na kupata faida nyingi". Alieleza Ndugu Asangye Bangu

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Wilaya ya Kilombero Ndugu Abraham Mwaikwila alisema kuwa suala la Stakabadhi Ghalani linatakiwa kuendele a kuelimishwa zaidi kwa Wananchi na Wakulima ndani ya Wilaya ya Kilombero ili iweze kuwasaidia Wananchi kuondokana na umaskini kwa wakulima na kupata faida zaidi

Latest Announcements

  • TANGAZO LA MAOMBI YA MPIGA KURA KUPIGA KURA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KATIKA KITUO TOFAUTI NA KITUO ALICHOJIANDIKISHA

    read more
  • TANGAZO LA ULIPAJI WA ADA NA USHURU KWA WANANCHI, WAFANYABIASHARA NA TAASISI MBALIMBALI IFAKARA MJI

    read more
  • View More

Habari Mpya

  • BENKI YA CRDB YAKABIDHI VITI NA MEZA 100 SHULE YA SEKONDARI MAHUTANGA
  • CHUO KIKUU CHA SOKOINE CHA KILIMO (SUA) KUWEZESHA VIJANA KUONGEZA UZALISHAJI NA MNYORORO WA THAMANI WA MAZAO - HALMASHAURI YA MJI IFAKARA
  • KAMATI YA USALAMA YA WILAYA YA KILOMBERO (KU) YAMPONGEZA MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MJI IFAKARA BI . PILLY KITWANA KWA USIMAMIZI MZURI WA MIRADI YA MAENDELEO
  • WAZEE WATAKIWA KUENDELEA KUDUMISHA AMANI NCHINI
  • WADAU WA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI WATAKIWA KUWASAIDIA WANANCHI KUPATA MBEGU BORA
  • More

Mawasiliano Yetu

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji Ifakara
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Simu ya Mkononi: -

Kurasa za Haraka

  • CHF
  • Ramani ya halmashauri ya mji wa Ifakara
  • MATOKEO KIDATO CHA NNE 2024
  • BOFYA HAPA KUOMBA KITAMBULISHO CHA WAJASILIAMALI WADOGO
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2024

Kurasa Mfanano

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Wizara ya Tamisemi
  • Wizara ya utumishi wa uma
  • Tovuti ya mkoa wa Morogoro
  • Tovuti ya Ajira Tanzania

Mitandao ya Kijamii

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya Uhifadhi
  • Maswali ya mara kwa mara
  • Ramani