WAFANYABIASHARA WAPEWA TAHADHARI DHIDI YA KIPINDUPINDU
Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Mhe. Dunstan Kyobya amewaasa wafanyabiashara wa Soko Kuu la Ifakara juu ya kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Kipindupindu.
Ameyasema hayo leo Januari 16,2024 katika Mkutano wa wazi na Wafanyabiashara hao.
"Tuzingatie kanuni za Afya ili kijikinga dhidi ya mlipuko wa ugonjwa huu kwani ni hatari na husababisha athari kubwa katika jamii". Amesema DC Kyobya.
Hata hivyo amezitaja kanuni za Afya zinazopaswa kufuatwa ikiwa ni pamoja na; kunawa Mikono kabla na baada ya kula, kuosha matunda kabla ya kula, kunawa Mikono kwa Maji tiririka na sabuni mara baada ya kutoka chooni, kutumia choo bora na kutupa kinyesi cha mtoto katika choo bora.

