• Nukuu ya Ukaribisho
  • Maswali ya mara kwa mara
  • Mawasiliano Yetu
Ifakara Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
Halmashauri ya Mji Ifakara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dira na Dhamira
    • Historia
    • Taswira
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Biashara
    • Ukaguzi wa Ndani
    • Manunuzi & Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Ustawi wa Jamii
    • TEHAMA
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Hatua
    • Ripoti
  • Uwekezaji
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Kapu
    • Utamaduni,Sanaa & Michezo
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Videos

VIZIMBA MAALUM VYA KUTUPA MAKOPO YA VIUWATILIFU VYATAKIWA KUJENGWA KATIKA KATA ZA HALMASHAURI YA MJI IFAKARA.

Posted on: June 5th, 2025

Na: Nuru Mangalili - Ifakaratc , Habari


Vizimba Maalum kwaajili ya Kutupa Makopo ya Viuwatilifu vimetakiwa kujengwa katika kila Kata za Halmashauri ya Mji Ifakara ili kuweka udhibiti bora wa utunzaji wa taka ndani ya Halmashauri.

Hayo yamesemwa leo Alhamisi Juni 5, 2025 na Afisa Tawala wa Wilaya ya Kilombero Bw. Fabius Byamungu aliyekuwa akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Mhe. Wakili Dunstan Kyobya wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambayo kihalmashauri  iliadhimishwa kwa kufanya Usafi katika Soko Kuu la Ifakara lililopo Kata ya Ifakara.

Awali aliwataka Wananchi kuhakikisha wanakabiliana na changamoto za utunzaji wa Mazingira kwa kuwa kwa sasa Dunia imekuwa ikikabiliwa na changamoto mbalimbali za uharibifu wa mazingira zinazotokana na kuongezeka kwa shughuli za kibinadamu   ikiwemo utupaji hovyo wa taka ngumu na plastiki, ukataji holela wa miti na uchomaji wa misitu hivyo kusababisha madhara mbalimbali kama uwepo wa magonjwa hatarishi kama kansa kutokana na utupaji holela wa taka hatarishi kama chupa za viuwatilifu katika vyanzo vya maji na utumiaji wa chupa hizo majumbani kwa shughuli mbalimbali kama utunzaji wa mafuta ya kula, chumvi ,maji n.k uharibifu wa vyanzo vya Maji, ardhi kupoteza ubora na kupungua uwezo wa kuzalisha, upotevu wa viumbe hai wa ardhini na majini , ongezeko ya hali ya jangwa na ukame n.k.


Afisa Tarafa wa Ifakara Bw. Fabius Byamungu akizungumza na Wafanyabiashara wa Soko Kuu Ifakara  juu ya Utunzaji wa Mazingira wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani


“Ili kukabiliana na changamoto za Utunzaji wa Mazingira na  rasilimali wananchi wa Ifakara tunaowajibu wa kuhakikisha tunalinda na kutunza  mazingira kwa kuzuia matumizi ya plastiki kuwa kibebeo cha bidhaa dukani, sokoni, buchani, n.k kuzuia utupaji hovyo wa makopo ya plastiki, ukataji miti hovyo na uvamizi wa maeneo ya hifadhi”. Alisema Bw. Byamungu na kuongeza “utupaji wa makopo ya viuwatilifu ufanyike  kwenye vizimba maalumu ili kuweka utunzaji wa taka,   hivyo kila Kata ijenge Kizimba maalum kwaajili ya kutupa makopo ya viuwatilifu. Alimaliza  Bw. Byamungu

Kwa upande wake Afisa Mazingira wa Halmashauri ya Mji Ifakara Bi. Salome Mayenga aliwasisitiza Wananchi wa Ifakara kuhakikisha  wanawajibika kutunza mazingira kwa kufanya usafi katika maeneo yao kila  mara na kuepuka matumizi ya plastiki.

Kauli mbiu katika Maadhimisho hayo kwa Mwaka huu ni “Mazingira Yetu na Tanzania Ijayo, Tuwajibike Sasa , “ Dhibiti Matumizi ya Plastiki”.

****MWISHO*****

Latest Announcements

  • TANGAZO LA MAOMBI YA MPIGA KURA KUPIGA KURA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KATIKA KITUO TOFAUTI NA KITUO ALICHOJIANDIKISHA

    read more
  • TANGAZO LA ULIPAJI WA ADA NA USHURU KWA WANANCHI, WAFANYABIASHARA NA TAASISI MBALIMBALI IFAKARA MJI

    read more
  • View More

Habari Mpya

  • BENKI YA CRDB YAKABIDHI VITI NA MEZA 100 SHULE YA SEKONDARI MAHUTANGA
  • CHUO KIKUU CHA SOKOINE CHA KILIMO (SUA) KUWEZESHA VIJANA KUONGEZA UZALISHAJI NA MNYORORO WA THAMANI WA MAZAO - HALMASHAURI YA MJI IFAKARA
  • KAMATI YA USALAMA YA WILAYA YA KILOMBERO (KU) YAMPONGEZA MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MJI IFAKARA BI . PILLY KITWANA KWA USIMAMIZI MZURI WA MIRADI YA MAENDELEO
  • WAZEE WATAKIWA KUENDELEA KUDUMISHA AMANI NCHINI
  • WADAU WA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI WATAKIWA KUWASAIDIA WANANCHI KUPATA MBEGU BORA
  • More

Mawasiliano Yetu

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji Ifakara
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Simu ya Mkononi: -

Kurasa za Haraka

  • CHF
  • Ramani ya halmashauri ya mji wa Ifakara
  • MATOKEO KIDATO CHA NNE 2024
  • BOFYA HAPA KUOMBA KITAMBULISHO CHA WAJASILIAMALI WADOGO
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2024

Kurasa Mfanano

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Wizara ya Tamisemi
  • Wizara ya utumishi wa uma
  • Tovuti ya mkoa wa Morogoro
  • Tovuti ya Ajira Tanzania

Mitandao ya Kijamii

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya Uhifadhi
  • Maswali ya mara kwa mara
  • Ramani