VIKUNDI MBALIMBALI HALMASHAURI YA MJI IFAKARA WAPATIWA ELIMU YA FEDHA.
Wataalamu kutoka Wizara ya fedha,Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na wadau wa sekta ya fedha wametoa elimu ya huduma za kifedha kwa makundi mbalimbali ikwemo Bodaboda,vijana wanawake na wenye ulemavu katika Halmashauri ya Mji Ifakara kwa lengo la kuleta uelewa wa usimamizi na matumizi ya fedha,namna ya utafutaji wa mitaji na uwekaji wa akiba.
Aidha vikundi hivyo vimetakiwa kuhakikisha wanatumia taasisi za huduma ndogo za fedha ambazo zimeidhinishwa kufanya shughuli za utoaji wa mikopo kwa mujibu wa Sheria.



