• Nukuu ya Ukaribisho
  • Maswali ya mara kwa mara
  • Mawasiliano Yetu
Ifakara Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
Halmashauri ya Mji Ifakara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dira na Dhamira
    • Historia
    • Taswira
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Biashara
    • Ukaguzi wa Ndani
    • Manunuzi & Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Ustawi wa Jamii
    • TEHAMA
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Hatua
    • Ripoti
  • Uwekezaji
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Kapu
    • Utamaduni,Sanaa & Michezo
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Videos

UJENZI WA SOKO JIPYA LA KIBEREGE KUKAMILIKA HIVI KARIBUNI

Posted on: January 12th, 2025

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Ifakara Mhe. Kassim Faya Nakapala amesema Ujenzi wa Soko la Kiberege katika  Kata ya Kiberege Halmashauri ya Mji Ifakara unatarajiwa kukamilika hivi Karibuni kutokana na  mradi huo kuendelea kutengewa bajeti ili kukamilisha ujenzi wake kwa Mwaka  Mpya wa Fedha  2025/2026.


Hayo ameyasema  Jumamosi tarehe 11 Januari 2025 wakati  akijibu swali lililoulizwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi ( CCM) Wilaya ya Kilombero  Ndugu, Mohammed Msuya kuhusu maendeleo ya Mradi huo wakati wa  Mkutano Mkuu wa Halmashauri  Kuu ya CCM Wilaya ya Kilombero kupitia Utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi.


Akijibu swali hilo Mhe. Nakapala alisema mpka sasa  Mradi huo wa Soko la Kiberege tayari umetengewa pesa  ya kukamilisha ujenzi wake katika bajeti ya mwaka 2025/ 2026 ambapo pesa hizo ni za Mapato ya Ndani ya Halmashauri na Mpaka kukamilika kwake Mradi utagharimu kiasi cha Shilingi Milioni 34,000,000.


 " Ili miradi ikamilike Halmashauri inatakiwa kuongeza kasi ya Ukusanyaji wa Mapato kwani Mradi huo ni miongoni  mwa miradi inayotegemea mapato ya ndani ili iweze kukamika ". Alisema Mhe. Nakapala


Sambamba na hilo , Mhe. Nakapala alieleza kuwa mpaka sasa Halmashauri imekusanya  kiasi cha Shilingi  2, 874,097,273 sawa na asilimia 44 ya Makusanyo ya Fedha za Mapato yote ya ndani ambayo lengo lake la Makusanyo kwa bajeti ya mwaka wa Fedha 2024 /2025 ni Sh. 6, 587,395,510.


Aidha Muheshimiwa Nakapala alieleza baadhi ya Changamoto zinazokabili Halmashauri katika ukusanyaji wa Mapato na kueleza kuwa tayari Halmashauri imeshaweka mikakati ya kuongeza wigo wa Ukusanyaji wa Mapato na kuahidi kufikia lengo la asilimia 100  ya Ukusanyaji wa Mapato ifikapo mwisho wa mwaka wa Fedha 2024/2025.









Latest Announcements

  • TANGAZO LA MAOMBI YA MPIGA KURA KUPIGA KURA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KATIKA KITUO TOFAUTI NA KITUO ALICHOJIANDIKISHA

    read more
  • TANGAZO LA ULIPAJI WA ADA NA USHURU KWA WANANCHI, WAFANYABIASHARA NA TAASISI MBALIMBALI IFAKARA MJI

    read more
  • View More

Habari Mpya

  • MAANDALIZI YA MPANGO MKAKATI WA HALMASHAURI KWA MWAKA 2026/27 HADI 20230/31
  • MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MJI IFAKARA, TIMU YA MENEJIMENTI WAPONGEZWA
  • MHESHIMIWA KASSIM FAYA NAKAPALA ASHINDA NAFASI YA MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA MJI IFAKARA
  • MHESHIMIWA KASSIM FAYA NAKAPALA ASHINDA NAFASI YA MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA MJI IFAKARA
  • KATIBU WA CHAMA CHA MAPINDUZI WILAYA YA KILOMBERO AWATAKA MADIWANI KUHAKIKISHA KERO ZA WANANCHI ZINATATULIWA
  • More

Mawasiliano Yetu

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji Ifakara
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Simu ya Mkononi: -

Kurasa za Haraka

  • CHF
  • Ramani ya halmashauri ya mji wa Ifakara
  • MATOKEO KIDATO CHA NNE 2024
  • BOFYA HAPA KUOMBA KITAMBULISHO CHA WAJASILIAMALI WADOGO
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2024

Kurasa Mfanano

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Wizara ya Tamisemi
  • Wizara ya utumishi wa uma
  • Tovuti ya mkoa wa Morogoro
  • Tovuti ya Ajira Tanzania

Mitandao ya Kijamii

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya Uhifadhi
  • Maswali ya mara kwa mara
  • Ramani