TIMU YA MPIRA WA MIGUU YA HALMASHAURI YA MJI IFAKARA YATINGA FAINALI KIBABE, MASHINDANO YA SHIMISEMITA
Timu ya mpira wa miguu ya Halmashauri ya Mji Ifakara leo Jumatano 04, Septemba 2024 imetinga hatua ya fainali kwenye mashindano ya SHIMISEMITA 2024 yanayoendelea Jijini Mwanza.
Timu hiyo imeingia Fainali mara baada ya kuwaondosha timu ya Tanga Jiji kwa magoli 2 bila majibu kwenye mchezo wa Nusu Fainali .
Awali katika mchezo wa robo Fainali Timu hiyo iliichapa Temeke MC goli 2 kwa 0.
Katika mchezo wa fainali Timu ya Ifakara FC watakutana na timu ya Geita DC mchezo utakaochezwa hapo kesho katika kiwanja cha Nyamagana Jijini Mwanza.



