• Nukuu ya Ukaribisho
  • Maswali ya mara kwa mara
  • Mawasiliano Yetu
Ifakara Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
Halmashauri ya Mji Ifakara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dira na Dhamira
    • Historia
    • Taswira
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Biashara
    • Ukaguzi wa Ndani
    • Manunuzi & Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Ustawi wa Jamii
    • TEHAMA
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Hatua
    • Ripoti
  • Uwekezaji
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Kapu
    • Utamaduni,Sanaa & Michezo
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Videos

TCRA KUINOA IFAKARA MJI DHIDI YA UTAPELI WA MITANDAONI

Posted on: February 2nd, 2025

Kufuatia kukithiri Kwa wimbi la utapeli na wizi wa mitandaoni Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa mafunzo Kwa Madiwani,Viongozi wa Serikali za Mitaa,vijiji na Kata wa Halmashauri ya Mji Ifakara.

Semina hiyo ya Mapambano dhidi ya utapeli wa  Mitandaoni iliandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Kilombero Mhe.Abubakary Asenga ambapo alisema kuwa kumekuwa na wimbi la utapeli wa Mitandaoni katika jamii zetu.

Aidha Mhe. Asenga amesema kuwa lengo la kuwaita viongozi wa Serikali za Mitaa, vijiji na Madiwani ni kujadili Kwa pamoja ni namna gani wanaweza kutatua changamoto hii lakini pia kufikisha ujumbe Kwa jamii zinazowazungukuka kuhusu suala la utapeli na wizi wa Mitandaoni.

Hata hivyo Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kilombero SP Daudi Nkuba  ameitaka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuwadhibiti watoa huduma za kusajili line ambao wamekuwa chanzo kikubwa cha uwepo wa  vijana wanaojikita katika kutafuta pesa kwa njia zisizofaa maarufu kama (Halohalo).

"hakuna uhalifu unaotuumiza Ifakara na Kilombero kama halohalo,sasa hivi kumekuwa na wimbi kubwa la vijana wakijishughulisha na vitendo hivi vya uhalifu wa Mitandaoni na Kuna baadhi ya Wazazi au walezi ambao wanachochea watoto wao kufanya wizi huu," Alisema SP Nkuba.

Meneja wa kitengo cha masuala ya wateja na watumiaji wa huduma za Mawasiliano (TCRA) mhandisi Kadaya Baluhye Amesema kuwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania haijihusishi na Michezo yeyote ya bahati na sibu pia Kuna umuhimu wa Wazazi kufuatilia tabia na mienendo ya watoto wao ili kudhibiti kujikita katika makundi yasiyofaa.

"Ulinzi na Usalama ni jukumu letu sote, Mbunge anataka kuwa na jamii inayofaa ndio maana tumekuja kutoa elimu hii Kwa wakazi wa Halmashauri ya Mji Ifakara Kila mmoja ana wajibu wa kulinda na kutumia Mawasiliano Kwa ufasaha

Naye Mkuu wa Wilaya Kilombero Mhe.Wakili Dunstan Kyobya amesema kuwa  anahitaji Ifakara ibadilike Kwa Kila Kijiji na Mtaa kuwe na daftari la wakazi ili kuweza kutambuana,Sambamba na hilo amesisitiza viongozi waliohudhuria semina hiyo kwenda kuwa mabalozi na kutoa Elimu Kwa jamii dhidi ya utapeli wa Mitandaoni.

 








Latest Announcements

  • TANGAZO LA MAOMBI YA MPIGA KURA KUPIGA KURA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KATIKA KITUO TOFAUTI NA KITUO ALICHOJIANDIKISHA

    read more
  • TANGAZO LA ULIPAJI WA ADA NA USHURU KWA WANANCHI, WAFANYABIASHARA NA TAASISI MBALIMBALI IFAKARA MJI

    read more
  • View More

Habari Mpya

  • BENKI YA CRDB YAKABIDHI VITI NA MEZA 100 SHULE YA SEKONDARI MAHUTANGA
  • CHUO KIKUU CHA SOKOINE CHA KILIMO (SUA) KUWEZESHA VIJANA KUONGEZA UZALISHAJI NA MNYORORO WA THAMANI WA MAZAO - HALMASHAURI YA MJI IFAKARA
  • KAMATI YA USALAMA YA WILAYA YA KILOMBERO (KU) YAMPONGEZA MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MJI IFAKARA BI . PILLY KITWANA KWA USIMAMIZI MZURI WA MIRADI YA MAENDELEO
  • WAZEE WATAKIWA KUENDELEA KUDUMISHA AMANI NCHINI
  • WADAU WA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI WATAKIWA KUWASAIDIA WANANCHI KUPATA MBEGU BORA
  • More

Mawasiliano Yetu

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji Ifakara
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Simu ya Mkononi: -

Kurasa za Haraka

  • CHF
  • Ramani ya halmashauri ya mji wa Ifakara
  • MATOKEO KIDATO CHA NNE 2024
  • BOFYA HAPA KUOMBA KITAMBULISHO CHA WAJASILIAMALI WADOGO
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2024

Kurasa Mfanano

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Wizara ya Tamisemi
  • Wizara ya utumishi wa uma
  • Tovuti ya mkoa wa Morogoro
  • Tovuti ya Ajira Tanzania

Mitandao ya Kijamii

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya Uhifadhi
  • Maswali ya mara kwa mara
  • Ramani