• Nukuu ya Ukaribisho
  • Maswali ya mara kwa mara
  • Mawasiliano Yetu
Ifakara Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
Halmashauri ya Mji Ifakara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dira na Dhamira
    • Historia
    • Taswira
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Biashara
    • Ukaguzi wa Ndani
    • Manunuzi & Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Ustawi wa Jamii
    • TEHAMA
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Hatua
    • Ripoti
  • Uwekezaji
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Kapu
    • Utamaduni,Sanaa & Michezo
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Videos

TAASISI MBALIMBALI ZAHIMIZWA KUJITOKEZA KUPANDA MITI ILI KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIA NCHI

Posted on: November 9th, 2024

Wadau  mbalimbali na Wananchi kwa ujumla wametakiwa kujitokeza kushiriki kupanda miti ili kukabiliana na mabadiliko ya Tabia ya Nchi.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Mhe. Wakili Dunstan Kyobya wakati akizindua  zoezi la upandaji miti la Shirika la SOLIDARMED katika eneo lililopo  pembezoni mwa Mto Lumemo lilipojengwa tuta kwaajili ya kuzuia mafuriko.

Aidha Tuta hilo limejengwa kuanzia  Kata  ya Mbasa hadi Kata ya Lipangalala kutokana na mafuriko yaliyotokea mwaka huu 5/5/2024 .

Katika kuendelea kukabiliana na mabadiliko ya Tabia ya Nchi , Shirika la SOLIDARMED limetengeneza bustani kwaajili ya Kupanda miti ya aina mbalimbali katika utunzaji wa mazingira na mabadiliko ya Tabia ya nchi .

" Niwapongeze SOLIDARMED kwa hatua hii na nikaribishe wadau mbalimbali waige mfano mzuri wa hawa wadau , waje wachukue eneo kwaajili ya bustani,  kila taasisi tuwe na bustani" . Alisema Mhe. Kyobya na kuongeza

" Kwa kufanya hivyo tunalinda Mto Lumemo na kuzuia kutokea kwa mafuriko.

Wakati huohuo,  Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara Bw. Said Majaliwa alilipongeza Shirika hilo kwa hatua hiyo na kusisitiza Wananchi kuendelea kupanda miti katika maeneo yao.

" Athari za mabadiliko ya Tabia ya Nchi kama tunavyojua huwa ni kubwa , hivyo kila mwananchi ashiriki katika suala Zima la utunzaji wa mazingira ". Alisisitiza Bw. Majaliwa

Kwa upande  wake , Mkurugenzi  wa Shirika la SOLIDARMED Dkt. Bernatus Sambili alisema Shirika hilo mbali na kufanya shughuli za Afya pia waliamua kushiriki kupanda bustani Ili kulinda Mazingira.

" Tutashiriki shughuli mbalimbali za ujenzi wa Taifa miongoni ni hii ambapo tutapanda miti zaidi ya 2000  katika eneo hili". Alieleza Dkt. Bernatus.


Latest Announcements

  • TANGAZO LA MAOMBI YA MPIGA KURA KUPIGA KURA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KATIKA KITUO TOFAUTI NA KITUO ALICHOJIANDIKISHA

    read more
  • TANGAZO LA ULIPAJI WA ADA NA USHURU KWA WANANCHI, WAFANYABIASHARA NA TAASISI MBALIMBALI IFAKARA MJI

    read more
  • View More

Habari Mpya

  • MAANDALIZI YA MPANGO MKAKATI WA HALMASHAURI KWA MWAKA 2026/27 HADI 20230/31
  • MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MJI IFAKARA, TIMU YA MENEJIMENTI WAPONGEZWA
  • MHESHIMIWA KASSIM FAYA NAKAPALA ASHINDA NAFASI YA MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA MJI IFAKARA
  • MHESHIMIWA KASSIM FAYA NAKAPALA ASHINDA NAFASI YA MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA MJI IFAKARA
  • KATIBU WA CHAMA CHA MAPINDUZI WILAYA YA KILOMBERO AWATAKA MADIWANI KUHAKIKISHA KERO ZA WANANCHI ZINATATULIWA
  • More

Mawasiliano Yetu

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji Ifakara
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Simu ya Mkononi: -

Kurasa za Haraka

  • CHF
  • Ramani ya halmashauri ya mji wa Ifakara
  • MATOKEO KIDATO CHA NNE 2024
  • BOFYA HAPA KUOMBA KITAMBULISHO CHA WAJASILIAMALI WADOGO
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2024

Kurasa Mfanano

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Wizara ya Tamisemi
  • Wizara ya utumishi wa uma
  • Tovuti ya mkoa wa Morogoro
  • Tovuti ya Ajira Tanzania

Mitandao ya Kijamii

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya Uhifadhi
  • Maswali ya mara kwa mara
  • Ramani