Rc Malima awatoa hofu Watumishi
Katika Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe.Adam Kighoma Malima, amewahakikishia Wafanyakazi kuwa Serikali sikivu inashughulikia changamoto zao kama kupandishwa Madaraja kwa wakati, ili kuboresha ufanisi katika Utendaji kazi.


Hata RC Malima ametoa vyeti vya pongezi kwa Wafanyakazi Hodari kwa Mwaka 2023/2024 kutoka Taasisi mbalimbali za Serikali za Mkoa wa Morogoro.


Maadhimisho hayo kimkoa yamefanyika katika Viwanja vya CCM Tangani ndani ya Halmashauri ya Mji Ifakara.