PAAF waagizwa kufuata miongozo
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara Bi.Zahara Michuzi, amewataka Wataalam wa usimamizi wa Malipo ya Walengwa wa Mpango wa Kaya maskini - TASAF kusimamia ugawaji wa fedha kwa kufuata miongozo sahihi.
Yamesemwa hayo leo Machi 26/2024 baada ya Halmashauri hiyo kupokea fedha Sh.243,533,000/= za kipindi cha Novemba - Disemba 2023 ambazo zinatolewa kwa Walengwa katika Vijiji/Mitaa 62 inayonufaika na Mpango huo.


