MWENYEKITI CCM WILAYA YA KILOMBERO AMEWATAKA WATAALAMU WA HALMASHAURI KUFANYA KAZI KWA WELEDI
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kilombero, Ndugu Mohammed Msuya, ametoa wito kwa wataalam kufanya kazi kwa weledi ili kuongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato kwa ajili ya kukamilisha miradi mbalimbali ya maendeleo,Kauli hiyo aliitoa tarehe 11 Januari 2025 wakati wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Kilombero, ambao ulijadili taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi.
Aidha alisisitiza umuhimu wa ushirikiano baina ya viongozi wa chama na serikali kama njia ya kuchochea maendeleo katika wilaya. Alieleza kuwa ushirikiano huo utaimarisha utekelezaji wa miradi na kuleta mafanikio ya haraka kwa jamii.




