MKUTANO WA KWANZA WA BARAZA LA MADIWANI HALMASHAURI YA MJI IFAKARA
Mkutano wa Kwanza wa Baraza la Madiwani Halmashauri ya Mji Ifakara umefanyika tarehe 4 Disemba 2025 katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimba uliopo Halmashauri ya Mji Ifakara.Katika tukio hilo Waheshimiwa Madiwani Wateule 26 walikula Kiapo cha Utii na Uadilifu mbele ya Mheshimiwa Hakimu Mkazi Mahakama ya Wilaya ya Kilombero Bestina Saning'o na Tamko la Kimaandishi kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara Bi. Pilly Kitwana .
Aidha Madiwani walisaini Fomu ya Ahadi ya Uadilifu kwa Viongozi wa Umma mbele ya Kamishna wa Maadili.
Katika Baraza hilo Wajumbe walimchagua Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Ifakara Mhe . Kassim Faya Nakapala kwa kura za ndiyo 21 katik ya kura 27 za Wajumbe zilizopigwa na kumchagua Mhe. Andrew Matajiri kuwa Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Ifakara kwa kupigiwa kura 21 za ndiyo kati ya Kura Halali 27 ambapo Hakuna Kura iliyoharibika.
Aidha Kamati za Kudumu za Halmashauri ya Mji Ifakara ziliundwa pamoja na kupitisha Ratiba za Vikao pamoja na kupokea taarifa ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara Bi. Pilly Kitwana kuhusu utekelezaji wa Shughuli za Halmashauri kipindi ambacho Baraza la Madiwani lilivunjwa.