MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MJI IFAKARA, TIMU YA MENEJIMENTI WAPONGEZWA
MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MJI IFAKARA NA TIMU YA MENEJIMENTI WAPONGEZWA
Katibu Tawala Msaidizi anayeshughulikia Mamlaka za Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro Bi. Neema Dachi amempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara Bi. Pilly Kitwana na Timu ya Menejimenti ya Halmashauri kwa kufanya vizuri katika Maeneo mbalimbali hususani wakati ambapo Baraza lilikuwa limevunjwa.
Pongezi hizo amezitoa Disemba 4, 2025 wakati wa Mkutano wa Kwanza wa Halmashauri uliofanyika katika Ukumbi wa Mlimba ulioko Halmashauri ya Mji Ifakara.

Bi. Neema amepongeza Halmashauri ya Mji Ifakara kwa kufanya Vizuri kwenye Ukusanyaji wa Mapato ambapo mpaka sasa imefikia asilimia 43 na kuwasihi kuongeza juhudi zaidi. Aidha alipongeza ununuiz wa Gari la Taka , kufanya vizuri kwenye Mwenge na Matokeo ya Darasa la Saba.
Wakati huohuo alimpongeza Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Ifakara Mhe. Kassimu Nakapala na Waheshimiwa Madiwani kwa kuchaguliwa na Wananchi kuwaongoza na kuwasisitiza kuishi katika Kiapo walichokula.
Aidha Bi. Neema alionya Juu ya Fedha mbichi na badala yake kuhakikisha Mapato yanayokusanywa yanapelekwa Benki kwa Wakati .
