MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MJI IFAKARA PILLY KITWANA ATEMBELEA BANDA LA HALMASHAURI YA IFAKARA MJI KUKAGUA MAANDALIZI YA MWISHO KUELEKEA MAONESHO YA NANE NANE 2025 KANDA YA MASHARIKI
Mkurugenzi wa Hlamashauri ya Mji Ifakara Bi. Pilly Kitwana leo Julai , 30 ,2025 ametembelea Banda la Maonesho ya Nane Nane la Halmashauri ya Mji Ifakara kukagua Hatua za Mwisho za Maandalizi ya Maonesho ya Nanenane Kanda ya Mashariki yatakayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu J. K. Nyerere kuanzia tarehe 1/8/2025 hadi tarehe 8/8/2025 Manispaa ya Morogoro.
Aidha Bi. Pilly Kitwana ametumia nafasi hiyo kuwakaribisha Wananchi wote kutembelea Banda la Halmashauri ya Mji Ifakara kwenye Maonesho hayo kwaajili ya kupata Elimu na Kujifunza Teknolojia za Kisasa katika Sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kutoka kwa Wataalam Mbalimbali.
Kauli Mbiu katika Maonesho hayo kwa Mwaka huu ni "Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo Mifugo na Uvuvi"